somo 18 katika supamaketi

 ongea na CRI
 

Ukifanya utalii nchini China, usisahau kuomba risiti ukipanda gari au kununua vitu, ili kujitetea haki wakati unapohitajika.Kwa sababu ukitaka kurudisha bidhaa, kutengeneza upya vitu vinavyoharibika, unatakiwa kuwa na risiti yake. Wakati unapopanda teksi, ukumbuke kumwomba dereva risiti kabla ya kushuka. Kwa kuwa ukipoteza vitu kwenye teksi, unaweza kutafuta risiti ili kupata nambari ya simu ya kampuni ya teksi na ukapiga simu na kupata vitu vyako ulivyovipoteza. Namna ya kuomba risiti? Baada ya kununua vitu, unaweza kumwambia mhudumu:"ma fan nin bang wo kai zhang fa piao, xing ma, xie xie." Mbali na hayo, ukishuka teksi unaweza kumwambia dereva:"wo yao fa piao."