-
Machungwa hayo ni matamu? Madukani au kwenye masoko hapa Beijing tunaweza kununua matunda ya aina mbalimbali. Kama unataka kununua machungwa, lakini una wasiwasi kuwa labda machungwa hayo si matamu, unaweza kumwuliza mwuza machungwa: zhe ju zi tian ma? Machungwa hayo ni matamu?
zhe, hayo, ju zi, machungwa, tian, tamu, ma, kisaidizi cha neno.
-
Kilo moja bei gani? Ukitaka kununua, unaweza kumwuliza bei. Unaweza kusema: duo shao qian yi gong jin? Duo xiao,ngapi, qian, hela, Duo xiao qian, bei gani,yi, moja, gong jin, kilo.
-
Sina pesa ndogondogo.
Kama huna pesa ndogondogo unaweza kusema: wo mei you ling qian. Sina pesa ndogondogo. Wo, mimi , mei you, sina, ling qian, pesa ndogondogo.
-
Nakupa noti ya yuan mia moja
gei, kupa, ni, wewe, yi zhang, noti moja. yi bai, mia moja, de, kisaidizi cha neno.