somo 19 katika soko la matunda

 ongea na CRI
 

Nchini China watu wakiongea, mara kwa mara huzungumzia bei za vitu na kuweza kuwauliza wengine: "Bei gani saa yako ya mkononi?" "Unapangishwa nyumba kwa bei gani kila mwezi?" "Matofaa hayo bei gani kilo moja?" Ukisikia maswali hayo usishangae. Kama usipotaka kumwambia, unaweza kusema:"wo wang ji le, nimesahau, au "wo bu zhi dao," Mimi sijui.