-
Nataka kuagiza pizza moja.
Kama ukitaka kuagiza pizza moja, unaweza kusema: wo yao ding ge bi sa bing.
Wo: mimi,
yao: kutaka,
ding: agiza,
ge: kisaidizi cha neno
bi sa bing: pizza.
-
Nitalipa kwa njia gani?
Zen me: kwa njia gani.
Fu: kulipa.
Qian: hela.
ne, neno la kisaidizi.
-
Unaweza kulipa baada ya kupokea pizza.
Ke yi huo dao fu kuan. Ke yi: weza, huo: chakula, dao: fika, fu: lipa, kuan: malipo.
-
Amua wewe saa ngapi.
Halafu unaweza kuuliza, chakula kitafikishwa kwako saa ngapi, na mhudumu anaweza kusema, amua wewe ifikie saa ngapi, "ni shuo yi ge shi jian." ni: wewe, shuo: sema, yi ge: moja, shi jian: wakati, saa.