somo 21 kununua vitu kwa simu

 ongea na CRI
 

Hivi sasa kutokana na maendeleo ya kasi ya biashara kwenye mtandao wa internet, watu wengi wanapenda kuagiza vitu kwa kupitia mtandao wa internet, kwani bei ya bidhaa huwa ni ya chini. Lakini wateja wanatakiwa kuelewa kuwa, wakinunua bidhaa kwenye mtandao wa internet wanaweza kuchagua kutokana na picha zilizowekwa kwenye tovuti, hivyo wakinunua lazima waombe kupewa risiti.
Kweli kama vitu walivyonunua vina tofauti kubwa na vile vilivyooneshwa kwenye mtandao wa internet, wataweza kutumia risiti hizo kuomba kuzirudisha. Wateja wanatakiwa kuchagua maduka yenye heshima kwenye mtandao wa internet ili kuagiza bidhaa zenye sifa nzuri, na kununua vitu kwenye mtandao wa internet hutumia credit kadi, hivyo kila wakinunua kitu kwenye tovuti, wanapaswa kubadilisha nambari za siri za kadi zao, na njia nzuri zaidi ni kulipa baada ya kupokea vitu ulivyogiza.