Wachina na watu wa nchi za magharibi wana desturi tofauti za chakula, watu wa nchi za magharibi wanazingatia zaidi virutubisho vya vyakula, wengi wao wanapenda kula mboga mbichi, kwani kula mboga mbichi kunaweza kuongeza vitamini mwilini.
Wachina wanapenda kula vyakula vyenye ladha nzuri, hivyo wakati wa kupika chakula kwa kukaanga au kuchemsha kwa muda mrefu, huwa baadhi ya virutubisho vinaweza kuharibika, lakini hivi sasa wachina wengi wanatilia maanani kudumisha virutubisho vya vyakula na pia wameanza kubadilisha mapishi yao ili kudumisha uwiano kati ya virutubisho na ladha ya vyakula.