-
Basi hili linaelekea kwenye eneo la makazi la Dongfang?
Zhe che: basi hili, dao: elekea, dong fang xiao qu: eneo la makazi la Dongfang, ma: kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Nataka kununua tiketi moja.
Na kama ukitaka kununua tiketi, unaweza kusema: mai yi zhang piao. Mai: nunua, yi zhang piao: tiketi moja.
-
Tafadhari tukifika kwenye kituo ninachoenda niambie. Kama unataka kondakta wa basi akuambie wakati wa kufika kwa kituo unachoenda unaweza kusema : dao le qing ni gao su wo. Dao le: kufika, qing: tafadhari, ni: wewe, gao su wo: uniambie.
-
Nipande basi lingine kwenye kituo gani?
Kama ulipanda basi lisiloenda moja kwa moja kwenye eneo dogo la Dongfang, na lazima ubadilishe basi, unaweza kumwuliza mhudumu wa basi: zai na er huan che? Zai na er: wapi, kwenye kituo gani, huan che: kupanda basi lingine.