somo 26 panda basi

 ongea na CRI
 

Wachina wengi ni wachangamfu sana ambao wanapenda kuwasaidia wengine, kuwasaidia wazee na watoto. Kwa mfano kwenye ofisi, kama mtu fulani akipata taabu wengine wanaweza kumsaidia kukabiliana na taabu hiyo; kwenye eneo la makazi, watu wa familia moja moja husaidiana, kama mtoto mmoja ambaye wazazi wake bado wako kazini, akirudi nyumbani baada ya masomo shuleni, huwa anaweza kufanya kazi ya masomo nyumbani nyumbani kwa jirani wa familia yake, hata kula chakula nyumbani kwa jirani wa familia yake.