-
Kuhusu mfumo wa matamshi ya maneno ya Kichina, kuna matamshi ya sauti tofauti kwenye ngazi ya kwanza, pili, tatu na nne, kwa mfano, 妈 (mā), 麻(má), 马 (mǎ), 骂 (mà),matamshi ya sauti tofauti kwenye ngazi ya kwanza, pili, tatu na nne, maana yao ya Kichina, 妈 (mā)mama, ni matamshi ya sauti kwenye ngazi ya kwanza, 麻(má)mkonge, au madoa,ni matamshi ya sauti kwenye ngazi ya pili, 马(mǎ) farasi, ni matamshi ya sauti kwenye ngazi ya tatu, 骂(mà) tukana, ni matamshi ya sauti kwenye ngazi ya nne. Matamshi ya maneno hayo manne kwa herufi ya kiswahili yote ni “ma”, lakini matamshi ya sauti ni tofauti na maneno na maana ni tofauti.
Kuthibitisha matamshi ya sauti kwenye ngazi tofauti ni muhimu sana. Kwani妈(mā) na 马(mǎ) kwa herufi ya Kiswahili yote ni “ma”, lakini 妈 (mā)maana yake ya kichina ni mama, na 马(mǎ)maana yake ya kichina ni farasi, ukisoma 妈(mā) ambayo matamshi yake ni kwenye ngazi ya kwanza kuwa 马(mǎ) ambayo matamshi yake ni ya ngazi ya tatu, maana yake itakuwa farasi, utasoma kwa makosa.
-
Mbele ya maneno ya jina kuna neno la kisaidizi kwa kuhesabu.
Mbele ya maneno ya jina kuna neno la kisaidizi kwa kuhesabu, kwa mfano, 一头牛(yì tóu niú),ng’ombe mmoja, 一(yì)moja, 头(tóu)neno la kisaidizi kwa kuhesabu, 牛(niú)ng'ombe. Unataka kusema一头牛(yì tóu niú)ng'ombe mmoja, ni lazima useme 一头牛(yì tóu niú), huwezi kusema ni 一牛(yì niú) bila kusema 头(tóu), neno 头(tóu), maana yake ya kichina ni kichwa, lakini ni neno muhimu la kisaidizi cha neno kwa kuhesabu.
Mnaposema mtu mmoja, mnasema 一个人(yí gè rén).一(yí),moja, 个(gè)vilevile ni kisaidizi cha neno kwa kuhesabu, 人(rén)mtu, ni lazima useme 一个人(yí gè rén),wakati wa kuhesabu, usiseme 一人(yí rén) bila kusema 个(gè) yaani kisaidizi cha neno kwa kuhesabu, kama ni watu wawili, unaweza kusema 两个人(liǎng gè rén), 两(liǎng )mbili, wawili, 个(gè)kisaidizi cha neno kwa kuhesabu, 人(rén)mtu; watu watatu, 三个人(sān gè rén).
-
Katika Kichina tunaunganisha maneno kuwa neno moja.
Hivyo neno moja la Kiswahili, kwa Kichina labda lina maneno mawili matatu au manne ndani yake. Kwa mfano garimoshi, 火车 (huǒchē),火 (huǒ)moto,车 (chē)gari. Volkano, 火山 (huǒshān),火(huǒ)moto,山 (shān) mlima .