Hivi leo miongoni mwa lugha zinazotumika duniani ni lugha ya Kichina peke yake tu ambayo haitumii herufi za alfabeti. Kuna masimulizi mengi miongoni mwa wachina kuhusu chanzo cha lugha ya Kichina. Inasemekana kwamba hapo kale kulikuwa na mtu mmoja anayeitwa Cang Jie ambaye alipata msukumo wa kutunga maneno ya Kichina kutokana na alama za nyayo za ndege na wanyama kwenye matope.
Baadaye wataalamu wa utafiti wa mabaki ya vitu vya kale waligundua vitu vingi vya kale katika makaburi yaliyoko karibu wa Mto Lingyang wa Wilaya ya Ju mkoani Shandong nchini China, na kwenye vyombo vya udongo waligundua maneno yaliyoandikwa kwa michoro ya picha. Kwa mujibu wa utafiti, maneno hayo yamekuwa na historia ya miaka 4500, ni maandishi ya mwanzo kabisa ya Kichina.
Ili kuwasaidia watu waweze kutambua na kutamka kwa usahihi maneno ya Kichina, mwaka 1958 serikali ya China ilitangaza “Mpango wa kutamka maneno ya Kichina kwa herufi za Kilatini”.
Mpango huo ni mfumo wa matamshi ya maneno ya Kichina kwa sehemu mbili za vokali na konsonanti, na herufi za vokali ni 21 na herufi za konsonanti ni 39.