Hivi sasa nchini China, watu wakienda posta si kama tu wanaweza kutuma barua, vifurushi, kutuma pesa, kununua kadi za barua na stempu, vilevile wanaweza kulipa gharama ya matumizi ya simu. Hata kwenye posta watu wanaweza kuweka akiba ya fedha. Shughuli za posta zinapanuliwa siku hadi siku, kila ifikapo sikukuu, posta pia zinaweza kuwasaidia watu kupeleka vyakula na maua ili kuwatakiwa heri na baraka jamaa na marafiki zao walioko mbali.