somo 36 Kutafuta nyumba

 ongea na CRI
 

Nchini China, kabla ya kufunga ndoa, vijana huishi pamoja na wazazi wao. Baada ya kufunga ndoa, baadhi yao bado wanaweza kuishi pamoja na wazazi wao, na wakipata watoto, wazazi wao wanaweza kuwasaidia kutunza watoto. Baadhi ya vijana wanapanga nyumba ama kununua nyumba na kuishi peke yao. Wakinunua nyumba wanaweza kulipa malipo mara moja, pia wanaweza kuomba mikopo kutoka benki ili kulipa kwa mafungu kila mwezi mpaka mwisho kutokana na mpango uliowekwa. Na familia zenye mapato ya chini na hali yao inalingana na ile iliyowekwa na serikali, zinaweza kutoa ombi la kununua nyumba zenye malipo ya chini kiasi, ama kupanga nyumba za malipo ya chini, lakini baada ya kutoa ombi zinatakiwa kusubiri ili kupata ruhusa.