-
Saa zimekuwa nyingi.
Baada ya kushiriki kwenye sherehe moja, giza limeingia na unataka kuondoka. Wakati huu unaweza kumwambia mwenyeji kuwa"shí jiān bù zǎo le." "shí jiān": wakati; "bù": si; "zǎo": mapema. "shí jiān bù zǎo le." yaani saa zimekuwa nyingi.
-
Tuondoke sasa.
Baada ya kusema "shí jiān bù zǎo le.", huenda unataka kusema "wǒ mén gāi zǒu le." Maana yake ni tuondoke sasa. "wǒ mén": sisi; "gāi": lazima; "zǒu le" : kuondoka.
-
Kwa heri!
Hii ni sentensi inayotumiwa mara kwa mara katika maisha yetu.
zài yaani tena, jiàn ni kuonana. "zài jiàn" maana yake ni kwa heri, au tutaonana tena.
-
Mzingatie afya!
Namna ya kusema Mzingatie afya kwa Kichina? Unaweza kusema: duō bǎo zhòng. Duō, maana yake ni nyingi. bǎo zhòng: kutilia maanani afya.
"duō bǎo zhòng" yaani Mzingatie afya. Ama pia unaweza kusema "bǎo zhòng".
-
Tuzidi kuwasiliana!
"Tuzidi kuwasiliana" kwa Kichina ni "bǎo chí lián xì"."bǎo chí": kudumisha."lián xì": mawasiliano.