somo 42 Kutuma pesa

 ongea na CRI
 

Nchini China kila ifikapo sikukuu, watu huweza kuwatumia pesa wazazi wao au jamaa na marafiki zao kwa ajili ya kuonesha kuwatakia mema. Hasa wakulima wanaofanya kazi za vibarua mijini, wengi kati yao wanawatumia pesa wazazi au jamaa zao ili kuwasaidia kumudu maisha au kuboresha maisha ya familia. Hivi sasa mabenki yameanzisha kazi ya kuwasaidia watu watoe mchango wa fedha wakati sehemu fulani ikikumbwa na maafa ya kimaumbile.