Zamani wachina walizoea kutumia pesa taslimu, hata wakienda kwenye sehemu nyingine kufanya kazi, ama kwenda nchi za nje kutalii walikwenda na pesa nyingi taslimu, hivyo mara kwa mara pesa za watu ziliweza kupotea au kuibwa. Lakini hivi sasa watu wengi wametambua ubora wa kutumia kadi ya benkini, hasa vijana wanaotumia kadi za benkini wanaongezeka zaidi, na mabenki mbalimbali pia yanawahamasisha watu watumie kadi zao. Ndiyo maana, si hali ya ajabu kwa mtu mmoja kuwa na kadi kadhaa benkini.