Baadhi ya watu wanaona matibabu ya kichina hupata ufanisi pole pole, hivyo matibabu hayo yanafaa zaidi kutibu ugonjwa sugu. Hali halisi ni kuwa, matibabu ya kichina yanaonesha pia umuhimu wake wakati wa kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa. Katika vitabu maarufu vilivyochapishwa katika zama za kale nchini China, mbinu za kutoa huduma ya kwanza kwa wagonjwa ni za aina mbalimbali kama vile kudunga sindano ya akyupancha, kufanya usingaji wa mwili, kushughulikia vizuri hali ya mifupa na kadhalika.