somo 55 Mazungumzo kati ya wanafunzi

 ongea na CRI
 

Vyuo vikuu vya China vimegawanyika kuwa vyuo vikuu vya masomo ya jumla, vya fizikia na uhandisi, vya kilimo na misitu, vya matibabu na dawa, vya ualimu, vya michezo ya riadha, vya Sanaa ya uchoraji, na vya maonesho ya michezo ya Sanaa. Kila mwaka mwanzoni mwa mwezi Juni, serikali ya China inaandaa mtihani wa pamoja wa kuwaandikisha wanafunzi wa vyuo vikuu vya kawaida kote nchini China, mtihani huo huitwa na watu kuwa ni高考( gao kao),yaani mtihani wa kiwango cha juu. Kwa kutegemea matokeo ya mtihani, wanafunzi wanaweza kuchagua vyuo vikuu. Hivi sasa, kuna vyuo vikuu zaidi ya 2000 kwenye sehemu mbalimbali nchini China. Mwaka 2007, idadi ya wanafunzi wa vyuo vikuu ilizidi milioni 27.