somo 57 Kujiandikisha

 ongea na CRI
 

Nchini China vyuo vikuu vingi, kila kimoja kina wito wake wa chuo ambao huonesha historia ya chuo na utamaduni wenye mtindo pekee. Kwa mfano, wito wa Chuo kikuu cha Beijing ni “Uzalendo, maendeleo, demokrasia, sayansi”, ambao umeonesha historia ya kujipatia uhuru kwa wanafunzi wa chuo hicho. Na wito wa Chuo kikuu cha Qinghua cha China ni “Kujiendeleza bila kulegalega, kufuata nidhamu na maadili na kutoa mchango kwa jamii”, wito huo wa chuo ulitokana na kitabu maarufu cha zama za Zhou za China ya kale kiitwacho “Zhou Yi”, ambacho kinasifiwa kuwa ni kitabu kilichokusanya busara na uhodari wa taifa la China. Na wito wa Chuo kikuu cha Fudan cha Shanghai ni “Kuwa na ujuzi mwingi na nia imara, kuwa na fikra zenye kiini zinazofuata hali halisi”, wito huo ulitokana na Kitabu maarufu cha “Lun Yu” ambacho kilinukuu maneno mengi ya Confucius ambaye alikuwa mwanafikra, mwanasiasa, na mwanaelimu maarufu wa zama za kipindi cha mwisho cha Chunqiu za China ya kale, pamoja na maneno waliyosema wanafunzi wa Confucius.