somo 59 Katika Jumba la dansi

 ongea na CRI
 

Hivi sasa nchini China vijana wengi wanapenda kwenda disco kuimba nyimbo na kucheza dansi, pia kutazama maonesho ya michezo ya Sanaa, ambapo vijana wanakunywa pamoja, kupiga soga ama kucheza dansi za disco zenye mtindo wa kuyumbayumba vilivyo. Mjini Beijing, katika sehemu za disco zenye mfumo wa kiwango cha juu wa kupaaza sauti na vifaa na zana za kisasa za taa na umeme, watu wanaweza kujionea mtindo wa kisasa wa kupiga muziki wa China kwa vinanda vya kielektroniki, na vijana wengi wanapenda kuandaa tamasha lao mwishoni mwa mwaka au mwanzoni mwa mwaka kwenye sehemu za disco.