-
Haloo,tafadhali niambie wewe ni nani?
Wachina wanapopiga simu huzoea kusema kwanza "wei" kama Haloo kwa Kiingereza. -
Lini utakuwa na nafasi? Kama ukitaka kwenda nje pamoja na rafiki yako, utamwuliza "ni shen me shi hou you kong?" ni, wewe; shen me shi hou, lini; you kong, kuna nafasi.
-
Kama unataka kukutana na rafiki yako, unaweza kumwuliza: wo men ji dian jian mian? Zai na er jian mian? Tukutana saa ngapi ? Tukutane mahali gani? Wo men, sisi, ji dian, saa ngapi? Zai, kwenye, na er,wapi, jian mian, kukutana.