somo 65 Kufanya mazoezi katika asubuhi

 ongea na CRI
 

Kufanya mazoezi ya kujenga mwili asubuhi kumekuwa ni desturi ya wachina wengi katika maisha yao. Katika mabustani au kwenye viwanja kila mahali mijini, wazee kwa watoto, wanaume kwa wanawake wanatembeatembea, kukimbia, kuimba nyimbo au opera, kucheza dansi, kufanya mazoezi ya kujenga mwili, kucheza Wushu na kadhalika, hayo yote ni mazoezi ya kujenga mwili kwa wachina wakati wa asubuhi. Watalii kutoka nchi za nje wakija China huenda kwa mahsusi kutazama wachina wakifanya mazoezi ya kujenga mwili.