somo 67 Mashindano

 ongea na CRI
 

Michezo ya 29 ya Olimpiki ilifanyika kuanzia tarehe 8 hadi 24 Agosti mwaka 2008 Beijing, mji mkuu wa China. Hii ilikuwa ni mara ya kwanza kwa China kuandaa michezo ya Olimpiki ya majira ya joto.
Mashindano ya michezo mingi yalifanyika mjini Beijing, na miji ya Shanghai, Tianjin, Shenyang na Qinhuangdao ilisaidia Beijing kuandaa mashindano ya michezo ya soka, na mashindano ya mashua zenye matanga yaliandaliwa mjini Qingdao.