Mandhari Nzuri
MANDHARI NZURI YA KIMAUMBILE
China ina rasilimali nyingi za maumbile, licha ya Jiuzaigou, Zhangjiajie na Huanglong, ambazo zimeorodheshwa kuwa mabaki ya kimaumbile ya dunia, kuna sehemu nyingine zenye mandhari nzuri ya kimaumbile zikiwa ni pamoja na Guilin ya sehemu ya kusini magharibi, milima ya Changbai ya sehemu ya kaskazini mashariki, milima ya Wasichana Wanne ya mkoa wa Guzhou na misitu ya sehemu ya joto ya Xishuangbanna ya mkoa wa Yuannan pamoja na mandhari ya misitu ya minazi ya kisiwa cha Hainan pia ni mandhari nzuri ya kimaumbile.
MILIMA NA MITO YA GUILIN
Mji wa Guilin uko katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang, kusini magharibi ya China, hali ya hewa ya huko ni ya vuguvugu na yenye unyevunyevu; hakuna baridi kali katika majira ya baridi, wala joto kali katika majira ya joto, na katika majira yote ya mwaka miti na majani huonekana ya rangi ya kijani, wastani wa hali-joto kwa mwaka ni nyuzi 19 za sentigredi.
Guilin ina mazingira bora ya kimaumbile, kutokana na utafiti wa kijiolojia, Guilin ilikuwa bahari kubwa kabla ya miaka milioni 300. kutokana na kuhamahama kwa ardhi ya dunia, mawe ya chokaa yaliyokuwa chini ya maji ya bahari yaliinuka juu na kuwa ardhi, baada ya kupigwa na upepo, jua na mvua kwa miaka mingi, yakawa milima inayopendeza, mapango marefu ya kupendeza na mito iliyopita chini ya ardhi. Sura nzuri ya milima, mto Li, mashamba na vijiji vimekuwa mandhari nzuri ya pekee, ambayo vinajulikana kwa "Mandhari ya Guilin inatia fora duniani".
Guilin ni mji wa kale wenye historia ya miaka mingi, ambao uliojengwa miaka 2,110 iliyopita. Hivi sasa, Guilin ina sehemu 109 za hifadhi za vitu vya kali za ngazi za taifa, mkoa na mji. Mashairi yaliyotungwa na wasomi wa enzi mbalimbali ya kusifu milima na mto wa Guilin na sanamu za kibudha, yako katika mapango ya milimani, hususan yako katika Guihai na genge la Mo la mlima wa magharibi. Sehemu maarufu zenye mandhari nzuri katika mji wa Guilin ni pamoja na mlima wa Pilian, bustani ya nyota 7, chemchem ya Longsheng, mawe ya filimbi na mlima wa pua ya ndovu.
Hivi sasa, mji wa Guilin una mahoteli 28 ya ngazi ya nyota ya wageni, mashirika 18 ya utalii na watembelezaji na wakalimani wa lugha za nchi za kigeni wapatao zaidi ya 1,000. Katika miaka ya karibuni, ujenzi wa miundo-mbinu imekuwa ikikamilishwa hatua kwa hatua, hivi sasa kuna njia ya safari za ndege zaidi ya 40 zinazofika kwenye miji mikubwa ya nchi za nje.
MLIMA WA CHANGBAI
Mlima wa Changbai uko katika mkoa wa Jilin, sehemu ya kaskazini mashariki ya China, ambayo ni mpaka kati ya nchi za China na Korea ya kaskazini na chanzo cha mito mitatu ya Tumen, Yalu na Songhua. Misitu minene isiyo na upeo pamoja na ndege na wanyama adimu wanaoishi ndani yake, imefanya mlima huo kuorodheshwa kuwa hifadhi ya viumbe ya umoja wa mataifa duniani katika mwaka 1980. hivi sasa, mlima wa Zhangbai umethibitishwa kuwa sehemu ya mandhari nzuri ya taifa ya ngazi ya 4A.
Mlima wa Changbai ambao unajulikana kwa "mlima wa kwanza wa sehemu ya kaskazini mashariki", katika historia ulikuwa sehemu wanayokaa wakazi wa sehemu ya kaskazini mashariki, na pia ni sehemu ya kukua na kustawi kwa kabila la wa-man. Hivyo katika enzi ya Qing, sehemu hiyo ilichukuliwa kuwa ni sehemu takatifu. Mlima wa Changbai unajulikana duniani kwa mandhari nzuri ya utalii, sehemu na kustawi kwa kabila la waman na mlima mtakatifu wa kabila la wakorea.
Mlima wa Changbai unajulikana kwa kuwa na rangi nyeupe kutokana na aina ya mawe meupe ya floatstone na theluji zilizoko katika kilele chake kikuu. Mlima huo ni uliumbwa kutokana na volkano, kutokana na data kuwa mlima huo ulilipukao mara tatu toka karne ya 16. Sura ya ardhi ni nzuri ajabu. Mandhari nzuri za mlima huo ni pamoja na ziwa la mbinguni, misitu ya mbetula, msitu ulioko chini ya ardhi, misonabari warembo, bonde kubwa, bustani iliyoko juu ya mlima, kilele kikuu, chemchem, mlango wa upepo mweusi na msitu wa floatstone.
Mlima wa Changbai una mazao ya jadi ya gen-seng, ngozi za marten, pembe za paa, licha ya hayo mlimani kuna raslimali za viumbe adimu zikiwa ni pamoja na misonobari warembo, mizabibu na uyoga mwitu, maua ya azelia, chui mkubwa na korongo wenye kichwa mwekundu.
Mawasiliano ya kwenda mlima wa Changbai ni mepesi sana, unaweza kupanda ndege kutoka Beijing, Shanghai na Shenyang hadi mji wa Jianji, halafu kufika huko kwa magari. Kuna mahoteli ya ngazi mbalimbali chini na juu ya mlima, chumba kizuri ni Yuan za Renminbi 220 kwa siku, na kitanda kimoja cha kawaida ni yuan toka 10 hadi 40 kwa siku.
MIJI MAARUFU YA UTALII NCHINI CHINA
China ni nchi kubwa yenye makabila mengi, ujenzi wa miji ya sehemu mbalimbali Una umaalumu wake. Katika sehemu ya kaskazini ya China kuna mji mkuu wa Beijing; sehemu ya mashariki kuna Shanghai, kitovu cha uchumi wa China; sehemu ya magharibi kuna mji wa LahSa wenye umaalumu wa kitibet; sehemu ya kusini kuna mji wa Kunming ambao hali ya hewa katika majira yote manne ya mwaka ni kama ya Spring. Miji mizuri iliyoendelea ni kama lulu zinazomeremeta katika ardhi ya China yenye kilomita za mraba milioni 9.6.
Hivi Sasa nchini China kuna miji 137 iliyothibitishwa kuwa miji bora ya utalii ikiwa ni pamoja na Shanghai, Beijing, Tianjin, Chongqing, Shenzhen, Hangzhou, Dalian, Nanjing, Xiamen, Guangzhou, Chengdu, Shenyang, Qingdao, Ningbo, Xian, Haerbin, Jinan, Changchun na Lasha. Licha ya hayo China imechagua miji 10 ikiwemo ya Haerbin, Jilin, Zhengzhou, Zahoqing, Liuzhou na Qingdao, kuwa miji maarufu ya kiutamaduni.
BEIJING
Beijing ni mji mkuu wa China, na ni kitovu cha siasa na utamaduni nchini China. Beijing iko katika sehemu ya kaskazini ya ardhi ya tambarare ya kaskazini ya China. Kijiografia, Beijing, Rome ya Italia, Madrid ya Hispania ziko katika latitudo moja. Hali ya hewa ya Beijing ni yenye upepo wa kimajira wa bara, siku za majira ya baridi na joto ni nyingi, siku za majira ya kichipuka na kupukutika ni kidogo na kukosa mvua. Wastani wa hali-joto ni nyuzi 11.8 sentigredi kwa mwaka.
Beijing ina historia ndefu sana ya kuanzia miaka 3,000 iliyopita. Katika kipindi cha mwaka 770 hadi mwaka 221 K.K, sehemu ya Beijing ilikuwa mji mkuu wa nchi ndogo za himaya ya ufalme, katika enzi za Qin na Han pamoja na kipindi cha Nchi Tatu, Beijing ilikuwa mmoja wa mji muhimu katika sehemu ya kaskazini ya China. Beijing ilianza kuwa mji mkuu wa nchi tangu enzi ya Jin, ikifuatiwa na enzi za Yuan, Ming na Qing, ambapo kulikuwa na wafalme 34 waliotawala dola kutokea Beijing.
Baada ya kuasisiwa China mpya, hususan katika miaka zaidi 20 iliyopita baada ya kuanza kutekeleza sera za mageuzi na ufunguaji mlango, sura ya Beijing ilikuwa na mabadiliko makubwa. Majengo ya kisasa yalijengwa kila mahali na uhusiano na nchi za nje ulikuzwa kwa mfululizo. Hivi sasa, Beijing, inapiga hatua kubwa kuingia kwenye kundi la miji mikubwa duniani. Beijing, ambayo mabaki ya historia yameungana vizuri na sura ya kisasa, inavutia watu wa sehemu mbalimbali. Katika miaka ya karibuni, Beijing kila mwaka imekuwa inapokea mamilioni ya watalii kutoka nchi za nje na milioni ya makumi ya watalii wa nchini.
Historia ndefu iliiachia Beijing vitu vingi vya kale pamoja na utamaduni murua wa jadi. Ikiwa unapenda vitu na mabaki ya utamaduni, unaweza kwenda kuona Ukuta Mkuu, kutembelea makasri makubwa, au kutembelea bustani za kifalme ambazo ni pamoja na Summer Palace, Beihai, Xiangshan na Tiantan. Mandhari nzuri na majengo makubwa ya huko yatafanya wewe kutoka kuondoka. Ikiwa unataka kufahamu utamaduni na mambo kuhusu watu mashuhuri wa China, unaweza kutembelea maskani mengi ya watu mashuhuri au kwenda kusikiliza Beijing opera. Ikiwa unataka kujua hali ya maendeleo ya maeneo mbalimbali ya siasa, uchumi, sayansi na teknolojia na kijeshi, unaweza kwenda kutembelea majumba ya makumbusho zaidi ya mia moja yaliyoko mjini Beijing. Ukitaka kujiburudisha kwa mandhari nzuri ya kimaumbile ya Beijing, unaweza kwenda kuangalia milima na mito iliyoko katika sehemu ya mzunguko wa Beijing.
Hivi sasa, sehemu za mandhari ya ngazi ya 4A zilizoko hapa Beijing ni pamoja na Tiantan, makaburi 13 ya enzi ya Ming, Summer Palace, Jumba la wanyama wa baharini la Beijing, Ukuta Mkuu wa Badaling, Mlima wa Jing, Bustan ya Beihai, bustani ya makabila ya China, Jumba la sayansi na teknolojia la China, bustani ya wanyama la Beijing na Bustani ya mimea ya Beijing.
X'IAN
Xi'an, ambayo iko katika sehemu ya kaskazini magharibi ya China, ni mji mkuu wa mkoa wa Shanxi na kuchukuliwa kuwa ni kitovu cha siasa, uchumi na mawasiliano cha sehemu ya kaskazini magharibi na China bara.
Mji wa Xi'an ni mmoja kati ya miji sita ya kale ya China ambayo ni Xi'an, Luoyang, Nanjing, Kaifeng, Hangzhou na Beijing. Xian ni mji mkuu wa enzi nyingi na kwa muda mrefu zaidi kuliko miji mingine ya kale, na kujulikana sana kwa historia na utamaduni wake. Katika historia ya China, wataalam wa elimu ya historia wamethibitisha kuwa enzi 10 za Zhou ya magharibi, Qin, Han ya magharibi, Zhao ya awali, Qin ya baadaye, Wei ya magharibi, Zhou ya kaskazini, Sui na Tang zilichagua Xi'an kuwa ni mji mkuu. Hivyo, mji wa Xian wenye historia ya zaidi ya miaka elfu moja, una athari kubwa katika historia na ni wa kipekee ukilinganishwa na miji mingine.
Xi'an, ambao unachukuliwa kuwa ni mmoja kati ya miji minne ya kale duniani, ni sehemu maarufu ya utalii. Sanamu za askari na farasi wa mfalme Qingshihuang, ambazo zinasifiwa kuwa ni "ajabu kubwa la nane duniani" ziko katika wilaya ya Lintong ya mji wa Xian, sanamu za askari na farasi ni zaidi ya 6,000 kwa jumla, na kuchukuliwa kuwa ni ugunduzi mkubwa kabisa wa karne ya 20. Licha ya hayo kuna sehemu nyingine za mandhari nzuri zikiwa ni pamoja na Mnara wa Wide Goose, Dimbwi la Huaqing, na mlima wa Hua. Picha hiyo ni Ukumbi wa makumbusho ya sanamu za askari na farasi za mfalme Qinshihuang.
LAHSA
Lahsa ni mji mkuu wa mkoa unaojiendesha wa Tibet, China, ambao uko katika upande wa kaskazini wa mlima wa Himalaya, eneo lake ni kilomita za mraba 29,052. hali ya hewa ya Lahsa ni ya uwanda wa juu, kuna siku nyingi zenye jua, mvua kidogo, hakuna baridi kali katika majira ya baridi wala joto kali katika majira ya joto, wastani halijoto katika mwaka ni sentigredi nyuzi 7.4; Mvua hunyesha katika miezi mitatu ya 7, 8 na 9, na kiwango cha mvua ni kiasi cha milimita 500; Jua linawaka kwa saa zaidi ya 3,000 kwa mwaka, hivyo Lahsa unajulikana kuwa ni "mji wa mwangaza". Lahsa ina hewa safi, jua nzuri, mchana ni joto kiasi na usiku ni baridi, hivyo ni sehemu nzuri sana ya kukwepa joto kali katika majira ya joto.
Lahsa iko katika uwanda wa juu wa Qinghai na Tibet, ambao unajulikana kama "paa la dunia", uko katika wastani wa mita 3,600 juu ya usawa wa bahari, hakuna hewa ya oxygen ya kutosha, ina upungufu wa hewa hiyo kwa kati ya 25% hadi 30% ikilinganishwa na sehemu nyingine za China bara. Katika siku za mwanzoni watu husikia maumivu ya kichwa na kupumua kwa haraka. Katika siku ya kwanza baada ya kufika Lahsa, mtu anapaswa kupumzika ili kuzoea hali ya huko. Kipindi cha kati ya mwezi Aprili na Oktoba ni kizuri kwa utalii huko Tibet. Katika lugha ya Kitibet, Lahsa ni mahali patakatifu anapokaa mungu. Mji wa Lahsa umekuwa na historia ndefu na jadi ya kidini, sehemu za utalii mjini ni pamoja na hekalu ya Dazhao, mtaa wa Baguo na kasri la Budala.
KIVUTIO CHA MIJI MIDOGO YA CHINA
Miji ya China ina historia ndefu, hususan baadhi ya miji midogo iliyojengwa zaidi ya miaka mia moja iliyopita, inavutia watu zaidi, kwa mfano, mto Li wa mkoa wa Yunnan umeorodheshwa kuwa ni urithi wa utamaduni duniani. Historia na utamaduni wa miji midogo pamoja na siku za jana na leo zimeanza kutembelewa na watalii wa nchini na wa nchi za nje.
TARAFA YA ZHOUZHUANG
Tarafa ya Zhouzhuang iko katika mkoa wa Jiangsu, sehemu ya mashariki ya China, umbali wa kilomita 38 tu kutoka mji wa kale wa Suzhou. Mchoraji mashuhuri wa michoro ya kichina Bw. Wu Guanzhong aliwahi kuandika makala ikisema kuwa Mlima Manjano umekusanya uzuri wa milima ya China, na tarafa ya Zhouzhuang imekusanya uzuri wa vijiji vyenye mito na maziwa", magazeti ya nchi za nje yanasifu Zhouzhuang kuwa ni "tarafa ya kwanza yenye mito na maziwa nchini China".
Tarafa ya Zhouzhuang inazungukwa na maziwa ya Deng, Baiyan, Dingshan, na Nan pamoja na mito ya wastani na midogo zaidi ya 30, nyumba za wakazi zote zimejengwa kando ya mito, ambazo ni nyumba za mtindo wa kale na zenye ua. Zaidi ya 60% nyumba za tarafa hiyo zilijengwa katika enzi za Ming na Qing, tarafa hiyo ya kale yenye kilomita ya mraba 0.4, ina nyumba za mtindo wa kale karibu 100, pamoja na malango makubwa zaidi ya 60 yaliyojengwa kwa matofali. Licha ya hayo, tarafa ya Zhouzhuang imehifadhi vizuri madaraja 14 yenye utaalamu wa kale, mandhari ambayo ni kama watu wanavyosema kuwa "madaraja madogo, mito na nyumba za wakazi". Mazingira ya Zhouzhuang ni mazuri na hayana makelele, hivyo ni sehemu nzuri za kusoma, wenyeji wa huko wana jadi ya kusoma, katika historia walijitokeza wasomi wakubwa zaidi ya 20. Wasomi na washairi wengi kutoka sehemu nyingine walitunga mashairi na kuchora michoro juu ya uzuri wa tarafa hiyo. Mfasihi wa enzi ya Jin ya magharibi Zahng Han, washairi wa enzi ya Tang Li Yuxi na Lu Guimeng waliwahi kukaa katika tarafa ya Zhou.
Mandhari muhimu ya tarafa ya Zhou ni pamoja na hekalu la Quanfu, chuo cha dini ya Dao cha Chengxu, Ukumbi wa Shen, daraja la Fuan na Jumba la mi. Tarafa ya Zhou iko katikati ya Suzhou na Shanghai, mawasiliano ni mepesi sana, kuna mabasi yanayofika huko moja kwa moja. Kwa kuwa Zhouzhuang iko karibu na Shanghai, hivyo, watalii wanaweza kwenda na kurudi kwa siku moja, huko hakuna mahoteli mengi ya ngazi ya nyota, lakini nyumba za kawaida za wageni ni nyingi, ingawa nyumba hizo siyo za hali ya juu, lakini ni safi sana.
MJI WA KALE WA PHOEINIX
Tarafa ya Phoenix iko katika wilaya inayojiendesha ya makabila ya watuju na wamiao, sehemu ya magharibi ya mkoa wa Hunan, katikati ya China."Mji wa kale wa Phoeinix" unaoitwa na mwandishi wa vitabu wa New Zealand Luis Ari kuwa ni mmoja wa mji mdogo nzuri kabisa nchini China, ulijengwa katika nasaba ya Kangxi ya enzi ya Qing. Mji huo unaojulikana kwa "Lulu ya magharibi ya mkoa wa Hunan" ni mdogo kweli kweli, na kuna barabara moja tu mjini humo.
Mji wa kale wa Phoenix una sehemu mbili za mji wa kale na mji mpya, mji wa kale uko kando ya mto, chini ya mlima, mto Tuo unapita katikati ya mji, ukuta mrefu wa mji ulijengwa kwa mawe mekundu kando ya mto, na mlima wa Nanhua uko karibu na mji wa kale. Ngome ya mji ulijengwa katika enzi ya Qing. Katika mto mpana ulioko karibu sana na mlango mkubwa wa kaskazini wa mji, lilijengwa daraja moja jembamba, watu wawili wakikutana kwenye daraja hilo, hawana budi kugeuza miili yao ili mmoja kumpisha mwenzie. Daraja hilo lilikuwa daraja pekee la kutokea nje kwa wakazi wa mji huo.
Tarafa ya Phoenix imejulikana kutokana na kuwa ni maskani ya mwanzo kabisa ya mwandishi vitabu mashuhuri Shen Congwen wa miaka ya karibuni. Maskani ya mwandishi vitabu huyo alikaa ndani sana ya kichochoro kimoja kilichotandikwa vipande vya mawe kwenye mtaa wa Ying wa mji huo wa kale. Nyumba yake ilijengwa kwa matofali na mbao ni kama nyumba ya kijadi ya Beijing. Sehemu muhimu ya mandhari ya tarafa ya Phoenix ni pamoja na kuangalia jua likichomoza katika mlima wa mashariki, misitu ya mlima wa Nanhua, makengele yakilia katika hekalu iliyojengwa mlimani, mashua za wavuvi zenye kandili katika usiku na kuangalia mbalamwezi kwenye daraja na Xi. Watalii wanaweza kuwasili mji wa Jishou mkoani Hunan kwa ndege kisha kutumia mabasi.
|