Utalii wa China
Hoteli Maarufu nchini China
ORODHA YA HOTELI MUHIMU ZA NYOTA TANO NCHINI CHINA
BEIJING
Hoteli ya Beijing Simu: 86-10-65137766 Anuani: Changanjie No. 33
Hoteli ya China simu: 86-10-65052266 Anuani: Jianguomenneidajie No. 1
Hoteli ya Ukuta Mkuu Simu: 86-10-65905566 Anuani: Dongsanhuanbeilu No. 10
Hoteli ya Kunlun Simu: 86-10-65003388 Anuani:
Xinyuannanlu No. 33
Hoteli ya Changfugong Simu: 86-10-65125555 Anuani: Jianguomenwaidajie No 26
Hoteli ya Guibinlou Simu: 86-10-65137788 Anuani: Dongchanganjie No. 35
Hoteli ya Shangrila Simu: 86-10-68512211 Anuani: Zizuyuanlu Haidian District
Hoteli ya Wangfu Simu: 86-10-65128899 Anuani: Jinyuhutong Dongcheng District
SHANGHAI
Hoteli ya XinJinjiang Simu: 86-21-64151188 Anuani: Changlelu No. 161
Hoteli ya Hilton Simu: 86-21-62480000 Anuani: Huashanlu No. 250
Hoteli ya Shangrila Pudong Simu: 86-21-68828888 Anuani: Fuchenglu Pudong No. 33
Hoteli ya Portmary No. 1376 Anuani: Nanjingxilu Jingan District
TIANJIN
Hoteli ya Sheraton Simu: 86-22-3343388 Anuani: Jinshanlu
GUANGZHOU
Hoteli ya Swain Simu: 86-20-81886968 Anuani: Shamiannanjie No.1
Garden Hotel Simu: 86-20-83338989 Anuani: Huanshidonglu No. 368
Hoteli ya China Simu: 86-20-86663388 Anuani: Liuhualu Yuexiu District
DALIAN
Hoteli ya Fulihua Simu: 86-411-82630888 Anuani: Renminlu No. 60
XI'AN
Hoteli ya Kaiyue Simu:86-29-7231234 Anuani: Dongdajie No. 158
Hoteli ya Sheraton Simu: 86-29-4261888 Anuani: Fenggaolu No. 12
MASHIRIKA MAARUFU YA UTALII
Hivi sasa nchini China kuna mashirika ya utalii 11,615 yakiwemo ya kimataifa 1,358 na ya nchini 10,257.
BEIJING
Shirika la Utalii la Kimatafa la China Simu: 86-10-85228866 Anuani: Dongdanbeidajie No. 1 Dongcheng District
Shirika la Utalii la China Simu: 86-10-64622288 Anuani: Beisanhuandonglu No. 2
Shirika la Utalii la Vijana la China Simu: 86-10-64656380 Anuani: Zuojiazhuanglu No. 1
Shirika la Utalii la Kanghui Simu: 86-10-65940885 Anuani: Nongzhanguannanlu No. 5
SHANGHAI
Shirika la Utalii la Kimataifa la Waihang la Shanghai Simu: 86-21-63500170 Anuani: Nanjingdonglu No. 800
Shirika la Utalii la Kimataifa la Yanhzi la Shanghai Simu: 86-21-62999403 Anuani: Caohejing Gulinlu No. 595
GUANGZHOU
Shirika la Utalii la Kimataifa la Tianma la Guangzhou Simu: 86-20-81881880 Anuani: Yanjiangxilu No. 113
XI'AN
Shirika la Utalii la Kimataifa la Elimu la Xi'an Simu: 86-29-5361018 Anuani: Cangannanlu No. 447
SHENZHEN
Shirika la Utalii la Kimataifa la Baoye la Zhenzhen Simu: 86-755-82101915 Anuani: Shennanzhonglu No. 1014
CHENGDU
Shirika la Utalii la Haiwai la Chengdu Simu: 86-28-86741113
Anuani: Shunchengdajie Shunji Plaza
Mambo kuhusu visa ya utalii nchini China
Ikiwa ni hatua ya kwanza kwa wewe kutembelea China, unapaswa kuishughulikia visa ya utalii. Wageni wanapaswa kuomba visa kwenye ofisi ya ubalozi ya China katika nchi za nje. Watalii zaidi ya 9 wakitaka kuitembelea China wanaweza kuomba visa ya utalii ya kikundi. Kwa wageni wanaotembelea mikoa maalumu ya kiuchumi ya Shenzhen, Zhuhai na Xiamen wanaweza kuomba visa ya utalii moja kwa moja kwa ofisi za forodha za mikoa hiyo. Wageni wale wanaotembelea mkoa wa Hainan kwa muda usiozidi siku 15, wanaweza kuomba visa kwenye ofisi za forodha za miji ya Haikou na Sanya. Wageni wanaotembelea Shenzhen kwa muda usiozidi saa 72 kutoka Hong Kong, hawana haja ya kuomba visa. Wageni waliopata visa wanatakiwa kuingia China kupitia forodha zilizofunguliwa kwa wageni au forodha walizoelezwa baada ya kushughulikiwa na wafanyakazi wa forodha.
Watalii wa kigeni wenye pasipoti na visa ya utalii wanaweza kufanya matembezi katika sehemu zilizosofungua mlango kwa nchi za nje, serikali ya China inalinda maslahi halali za wageni walioko nchini, lakini hawaruhusiwi kufanya shughuli zisizolingana na hali yao, zikiwa ni pamoja na ajira, kueneza dini na kufanya mahojiano na watu bila kibali, la sivyo watachukuliwa hatua. Aidha, wanapokuwa nchini China wanapaswa kuheshimu sheria na mila za China.
Watalii wanaweza kufanya matembezi nchini China katika muda waliopewa. Endapo wanataka kuendelea kufanya matembezi baada ya kupita muda wao, wanaweza kuziomba idara za usalama za karibu kurefusha muda wa matembezi. Baada ya kumaliza matembezi wanatakiwa kuondoka China kupitia forodha za kimataifa zilizofunguliwa kwa wageni.
Mambo unayopaswa kujua wakati unapopita kwenye forodha ya China
Mgeni anapopita kwenye forodha ya China anatakiwa kufuata maagizo husika ya forodha ya China, ili kufanikisha matembezi yako na kupita kwenye forodha bila matatizo, anatakiwa kufahamu mambo yafuatayo:
Mtalii anaondoka China akichukua au kusafirisha vitu vinavyo orodheshwa hapo chini, anatakiwa kuieleza forodha:
Vitu vinavyotozwa ushuru, na kiasi cha vitu vinavyoingia nchini bila kulipa ushuru
Vitu vinavyotumiwa na wasafiri wenyewe safarini pamoja na vitu ambavyo haviko katika eneo la vitu vinavyotumiwa na wasafiri wenyewe safarini, lakini bado vinahesabiwa kuwa ni vitu wanavyohitaji safarini;
Vitu vinavyopigwa marufuku kuingia au kutoka China pamoja na kiasi cha vitu vinavyoruhusiwa kuingia na kutoka China vikiwa ni pamoja na vitu vya kale, sarafu, dhahabu, fedha pamoja na vitu vilivyotengenezwa kwa madini hayo, maandishi yaliyochapishwa, na kaseti za audio na video;
Bidhaa, sampuli za bidhaa na vitu ambavyo haviko katika eneo la mizigo ya watalii.
NJIA ZA RANGI NYEKUNDU NA KIJANI
Wasafiri wanaotakiwa kulipa ushuru na wale waliohitaji kibali kwa mizigo yao wapite kwenye "njia nyekundu"; wasafiri wengine wanaweza kupita kwenye "njia ya rangi ya kijani".
KANUNI ZA KAWAIDA
Kwa kawaida, msafiri anapopita kwenye forodha, mizigo yote aliyokuwa nayo inatakiwa kukaguliwa. Mizigo ambayo haijakubaliwa na forodha haichukuliwi au kusafirishwa.
Mizigo yake iliyosafirishwa, ambayo haikuwa pamoja na msafiri inatakiwa kutolewa maelezo katika "fomu ya mizigo ya msafiri", na inatakiwa kuingia au kutoka nchini katika muda wa miezi 6 baada ya msafiri kuingia au kutoka China.
"Fomu ya mizigo ya msafiri" iliyosainiwa na mfanyakazi wa forodha inatakiwa kutunzwa vizuri ili ashughulikiwe haraka wakati atakapoondoka au kuingia nchini.
Aidha, msafiri anapaswa kutoa maelezo kwa forodha wakati anapoondoka China akichukua vitu vya mabaki ya kiutamaduni. Vitu vya mabaki ya kiutamaduni alivyonunua msafiri katika maduka yenye leseni ya biashara ya mabaki ya kiutamaduni, forodha inamruhusu kuondoka baada ya kukagua risiti maalumu za biashara hiyo yenye muhuri wa idara ya usimamizi wa mabaki ya kiutamaduni ya China. Msafiri akitaka kuondoka nchini na kuchukua vitu vya mabaki ya kiutamaduni ambavyo alivipata kwa njia nyingine vikiwa ni pamoja na kurithi kutoka wazazi au kupewa zawadi na marafiki, anapaswa kuthibitishwa na idara ya usimamizi wa vitu vya mabaki ya kiutamaduni ya China. Hivi sasa, idara hiyo imefungua ofisi zake katika forodha za miji minane ikiwemo ya Beijing, Shanghai, Tianjin na Guangzhou. Vitu vinavyoruhusiwa kuchukuliwa katika nchi za nje baada ya kuthibitishwa na kupewa kibali na idara ya usimamizi wa mabaki ya vitu vya kiutamaduni vinakubaliwa kupita kwenye forodha ya China.
MAELEZO KUHUSU KARANTINI
Idara ya karantini ya China ni idara ya utekelezaji wa sheria iliyoanzishwa kutokana na agizo la serikali kuhusu shughuli za karantini zinaohusika na nchi za nje, idara hiyo na vitengo vilivyo chini yake katika forodha zilizofunguliwa mlango kwa nchi za nje kufanya ukaguzi wa karantini kwa mujibu wa sheria juu ya watu wanaoingia na kutoka nchini, na forodha zinatoa ruhusa ya kuingia au baada ya kuona vyeti vilivyosainiwa na vitengo vya karantini.
Vyombo vya mawasiliano, watu, chakula, maji ya kunywa pamoja na wadudu na maradhi ya kuambukiza vinafuatiliwa zaidi.
Vitengo vya karantini vinawazuia wageni wenye baadhi ya magonjwa kuingia nchini, ambao ni pamoja na wenye virusi vya ukimwi, magonjwa ya zinaa ya kuambukiza na kifua kikuu kilichoko katika kipindi cha kuambukiza.
|