Sikukuu Muhimu za Makabila Madogo
akabila madogo ya China yana shughuli nyingi za kusherehekea sikukuu zao, karibu kila kabila lina sikukuu zao muhimu. Kwa mfano mwaka mpya wa kalenda ya kitibet wa kabila la Tibet, tamasha ya kumwaga maji ya kabila la Dai, sikukuu ya tochi ya kabila la Yi, tamasha ya March ya kabila la Bai, tamasha ya nyimbo ya kabila la Zhuang na tamasha ya Nadamu ya kabila la Mongolia. Baadhi ya serikali pia zimeziweka sikukuu za kikabila kuwa siku ya likizo, kama vile mwaka mpya wa kalenda ya kitibet na siku ya Idd El Hajj.
Sikukuu ya Id-el-haji
Siku ya Id-el-fitri ni sikukuu ya mwaka ya waislamu, maana ya Id-el-fitri ni kuchinja na kutoa sadaka, hivyo sikukuu hiyo pia inaitwa sikukuu ya "Corban", ni sikukuu ya kutoa sadaka. Sikukuu ya Id-el-fitri ni sikukuu ya pamoja ya makabila ya Hui, Uigur, Khasak, Uzbek, Tajik, Tataer, Kerkz, Shala, Dongxiang na Baoan yanayoamini kiislamu, ni tarehe 10 Desemba ya kalenda ya kiislamu. Waislamu husafisha nyumba zao na kupika vyakula vya keki kusherehekea sikukuu hiyo. Alfajiri ya sikukuu hiyo, waislamu wanatakiwa kuoga na kuchoma ubani kuvaa nguo safi na kwenda kufanya sala msikitini. Kila familia itachinga mbuzi, ngamia au ng'ombe kuwakaribisha wageni. Waislamu wanakula pamoja nyama za mbuzi na ng'ombe, keki na matunda, huku wakifanya mazungumzo. Kabila la Uigur la mkoa wa Xinjiang wanaposherehekea sikukuu ya Id-el-fitri hufanya tamasha kubwa ya nyimbo na dansi. Makabila ya Khazak, Kerkz, Tajik na Uzbek yanafanya mashindano ya kudaka mbuzi, kupanda farasi na kupigana mieleka.
Sikukuu ya Id-el-fitr
Sikukuu ya Id-el-fitr ni sikukuu ya makabila ya Hui, Uigur, Khazak, Uzbek, Tajik, Tataer, Kerkz, Shala, Dongxiang na Baoan, sherehe hufanywa mwanzoni mwa mwezi Oktoba wa kalenda ya kiislamu. Septemba ya kiislamu ni mwezi wa ramadhani, kipindi cha mfungo ni siku 29 au 30. Katika mwezi wa ramadhani, waislamu wanakula chakula kabla ya jua kuchomoka, mchana hawaruhusiwi kukula chakula, kunywa maji, hata kuvuta sigara. Isitoshe, waislamu wanatakiwa kuacha kujamiana na kuachilia mbali shauku yote katika mwezi wa ramadhani ili kuonesha imani yao kwa Allah. Watoto, wazee na wagonjwa hawana haja ya kufunga, wanawake pia wanaweza kuacha kufunga katika kipindi cha hedhi, lakini hawawezi kula chakula hadharani. Wagonjwa na wanaosafiri hawana haja ya kufunga, lakini wanatakiwa kufidia baadaye, au kutoa fedha na vitu. Usiku unapoingia, adhana ya msikiti ikilia, watu wanaweza kula chakula. Wakati huo wageni wanaosafiri wakiona njaa wanaweza kuomba chakula kwa wenyeji.
Shughuli za kusherehekea sikukuu ya Id-el-fitr ni kubwa na ya shangwe. Kabla ya kufika kwa sikukuu hiyo, watu hupaka rangi nyumba zao, kusafisha ua na kukatwa nywele. Vijana hufunga ndoa wakati huo.
Sikukuu ya Mwaka mpya ya Kalenda ya Kitibet
Sikukuu ya mwaka mpya ya kalenda ya Kitibet ni sikukuu muhimu kabisa kwa watu wa Tibet, sherehe hiyo hufanyika kwa siku 15 kuanzia tarehe mosi Januari ya kalenda ya kitibet. Siku ya kwanza ya mwaka mpya, inapopambazuka, vijana wa kike na kiume wanaovaa nguo maridadi husalimiana na kutakiana heri na baraka ya mwaka mpya. Watibet huenda kuabudu mabuda katika mahekalu, au kuimba nyimbo na kucheza dansi mtaani, lakini siku hiyo hawaruhusiwi kutembelea nyumbani mwa jamaa na marafiki.
Tamasha ya Nadam
Tamasha la Nadam ni sikukuu ya jadi ya wamongolia wanaoishi katika mikoa ya Mongolia ya ndani, Gangsu, Qinghai na Xinjiang, ambalo linafanyika katika mwezi wa Julai na Agosti kila mwaka. Maana ya Nadam kwa Kimongolia ni burudani au michezo. Tamasha la Nadam ina historia ndefu. Zamani shughuli za kutoa sadaka zilifanyika katika kipindi cha tamasha hilo, wa-lama walifanya ibada kwa kufukiza na kuwasha mishumaa, kuomba baraka na kuondoa balaa. Hivi sasa mambo muhimu ya Nadam ni kufanya michezo ya kienyeji kama vile mieleka, mashindano ya kupanda farasi na kulenga shabaha kwa mshale, au michezo ya riadha kama vile kupiga mbio, kuvuta kamba, kucheza mpira wa wavu na mpira wa kikapu.
|