8: Elimu, Sayansi na Teknolojia

Hali ya Jumla ya Elimu Nchini China

China ni nchi yenye idadi kubwa ya watu, na idadi ya watu wanaohitajika kuelimishwa pia ni kubwa. Hivi sasa China inashughulikia elimu kwa kiwango kikubwa kabisa duniani, sasa watu zaidi ya milioni 200 wanasoma katika shule za aina mbalimbali nchini China.

Elimu ya China imegawanya katika vipindi vya elimu ya chekechea, elimu ya msingi, elimu ya sekondari na elimu ya juu. Serikali ya China inatekeleza elimu ya lazima kwa miaka tisa kuanzia shule ya msingi hadi sekondari ya chini. Wanafunzi katika kipindi cha elimu ya lazima hawalipi karo, kila mwaka wanatakiwa kulipa Yuan mia kadhaa kwa ajili ya vitabu tu.

Serikali ya China inatilia maanani sana kuendeleza elimu ya lazima, hivi sasa asilimia zaidi ya 90 ya watoto wenye umri wa kwenda shule wanasoma shuleni. Katika miaka ya usoni, serikali ya China itatia mkazo kwenye kukuza elimu ya lazima vijijini na elimu ya juu, na kuwawezesha watoto wote wasome na kuanzisha vyuo vikuu vya kiwango cha kwanza duniani.

Sehemu kubwa ya elimu ya China inaendeshwa na serikali. Katika miaka ya hivi karibuni, elimu inayoendeshwa na watu binafsi imepata maendeleo, lakini kwa ujumla kiwango chake bado hakiwezi kulingana na kile cha serikali.


1 2 3 4 5 6 7