Dawa za Jadi ya Kichina
Dawa za jadi za kichina zinatumika katika kukinga na kutibu magonjwa zikiwa ni pamoja na za aina ya mimea, wanyama, madini na kemikali na baiolojia. Dawa za jadi za kichina zilivumbuliwa na kuanza kutumika milenia kadhaa zilizopita.
HISTORIA FUPI YA DAWA ZA KICHINA
Kuanzia kipindi cha Xia, Shang na Zhou (kiasi cha karne 22 kabla ya Kristo), nchini China kulikuweko na pombe ya dawa na dawa ya maji. Katika enzi ya Zhou ya Magharibi (kiasi cha karne ya 11 kabla ya Kristo) kilitungwa kitabu kilichojulikana kwa "Mashairi", ambacho ni cha kwanza chenye habari kuhusu dawa. Kitabu kingine kinachojulikana kwa "Neijing" ni kitabu cha nadharia ya tiba za jadi za kichina, ambacho kimeweka msingi kwa dawa za jadi za kichina.
Baada ya kuasisiwa kwa Jamhuri ya Watu wa China mwaka 1949, utafiti kuhusu elimu za mimea, uthibitishaji, kemikali na fizikia za dawa za jadi za kichina pamoja na tiba za jadi za kichina zimeendelezwa kwa nguvu. Kutokana na msingi wa kufanya uchunguzi mkubwa kuhusu chanzo cha dawa za kichina, kitabu kilichojulikana kwa "Orodha ya Dawa za Kichina" kilitungwa na kukamilika mwaka 1961, ambapo aina za dawa za kichina zimefikia 5767.
RASILIMALI ZA DAWA ZA KICHINA
China ina eneo kubwa, sura za ardhi na hali ya hewa za aina mbalimbali, hivyo ina mazingira za aina nyingi za asili, ambayo inaleta hali nzuri sana kwa ukuaji wa mimea ya dawa. Hivi sasa dawa za aina zaidi ya 600 kati ya dawa za kichina za aina zaidi ya 800 zinazopendwa na binadamu. Hivi sasa dawa za kichina zinasafirishwa kwa nchi zaidi ya 80 duniani na zimepata sifa nzuri.
UKUSANYAJI NA USINDIKAJI WA DAWA ZA KICHINA
Ukusanyaji wa dawa za kichina ni hatua muhimu katika uzalishaji na usindikaji wa dawa za kichina, mabingwa wa dawa za kichina wa zamani walisisitiza kukusanya mimea ya dawa katika wakati mwafaka. Kukusanya mimea ya dawa katika wakati mwafaka kunaweza kuongeza nguvu ya dawa na kupunguza sumu yake.
Mimea ya dawa baada ya kukusanywa haiwezi kutumika moja kwa moja ila tu baada ya kusindikwa kwa mbinu za aina mbalimbali.
MATUMIZI YA DAWA ZA KICHINA
Dawa za kichina zilianza kutumika toka miaka mingi iliyopita, hadi hivi sasa zinafanya kazi muhimu za kulinda afya za watu. Nadharia na uzoefu wa dawa za kichina vimeonesha umaalumu wa utamaduni wa China. Dawa nyingi za kichina ni za kimaumbile ambazo hazina sumu nyingi. Zikichanganywa pamoja na baadhi ya dawa nyingine mwafaka, nguvu yakezinaongezeka zaidi na sumu yake huwa ni ndogo zaidi.
MAENDELEO YA DAWA ZA KICHINA
Mwelekeo wa utafiti wa dawa za kichina katika siku za baadaye ni kujifunza uzoefu wa jadi wa uzalishaji wa dawa za kichina na kuotesha mbegu bora na kuzuia mimea ya dawa kuvia.
|