Jambo Lisilofahamika la Kale
Kuhusu Xu Fu Kwenda Japan
Baada a Qinshihuang kuwa mfalme wa enzi ya Qin, alitawaliwa na tamaa ya kuwa na maisha ya kudumu, alipata habari kuwa kuna mlima kwenye bahari ya Bo, ambapo kuna dawa zinazoweza kufanya mtu anayekula dawa hiyo kutofariki, hivyo alituma watu kwenda kutafuta dawa hiyo, lakini hawakuona dawa hiyo.
Lu Sheng alirudi na mikono mitupu, mfalme Qinshihuang akamtuma Xu Fu kwenda kuitafuta dawa hiyo tena. Xu Fu aliporudi kutoka baharini alimwambia mfalme kuwa aliona mlima wa Penglai na dawa hiyo pia, lakini viumbe waliokuwa wanaoishi kwenye mlima huo walimnyima na kusema kuwa zawadi aliyopeleka ni kidogo sana, na walisema kuwa mfalme akitaka dawa hiyo, sharti awapelekee wanaume, wanawake na mafundi hodari. Mfalme alifurahi sana baada a kusikia kuwa Xu Fu aliona dawa hiyo, akachagua watoto elfu 3 wa kike na wa kiume pamoja na mafundi hodari, alimtuma Xu Fu kwenda tena kwenye mlima wa huo. Xu Fu hakuona dawa hiyo, lakini aliogopa kurejea na kuonana na mfalme, hivyo aliongoza watu hao kwenda Japan na wakaanza kuishi huko. Hatimaye Xu Fu alifariki kwenye mlima wa Fuji nchini Japan.
Nchini Japan kuna hadithi na maandishi mengi ya kumbukumbu kuhusu Xu Fu, hata baadhi ya wanaelimu wanaona kuwa Xu Fu ndiye mwanzilishi wa nchi ya Japan, watu wa Japan vilevile wanamchukulia Xu Fu kama mtakatifu wa jadi na kumwabudu.
Uchimbaji wa Mapango ya Mogao
Mapango ya Mogao ni ya kwanza kwa ukubwa na kamilifu ya mabaki ya dini ya kibudha duniani. Hiyo kama bohari ya vitu va sanaa inayofuatiliwa na watu wengi duniani, kwa nini ilijengwa kwenye genge la mlima ulioko kwenye jangwa la Gobi, sehemu ya kaskazini magharibi ya China?
Inasemekana kuwa mahali palipochimbwa mapango ya Mogao huko Denghuang palichaguliwa na mtawa Yue Zun. Mwaka 366 Yu Zun katika matembezi yake alifika chini ya mlima wa Sanwei, wakati ule ulishakuwa jioni, lakini hakupata mahali pa kulala, alipokuwa akiwaza, ghafla alinyanyua kichwa na kuona maajabu kwamba kulikuwa na mwangaza wa rangi ya dhahabu kwenye mlima uliotazamana naye, na kama kulikuwa na budha walioonekana katika mwangaza. Yue Zun alishangazwa sana na kuona kuwa kumbe hapo ni mahali patakafitu! Hivyo alitafuta watu kuchimba kwenye genge la mlima huo, na kulikuwa na mapango zaidi ya 1,000 ktika enzi ya Tang.
Utafiti uliofanywa na wataalamu unaonesha kuwa uchimbaji wa mapango ya mawe ya Mogao ni mafanikio ya akili ya mababu jadi, mapango kuchaguliwa kuchimbwa kwenye jangwa ni kutokana na wazo la kuungana na mazingira ya kimaumbile na kutengana kati ya dini ya kibudha ya maisha na desturi ya binadamu.
Mabaki ya Bustani ya Yuanming Yako Wapi
Mwaka 1860 jeshi la mungano la Uingereza na Ufaransa lilivamia Beijing na kuingia bustani ya Yuanming, walichukua kila kitu chenye thamani. Vitu vya zawadi lilivyotoa jeshi la Ufaransa kwa mfalme wake baada ya kurejea nchini vilikuwa karibu elfu 10. Hivi sasa watu wakitaka kuona vitu vilivyokuwako katika bustani ya Yuanming hawana budi kwenda nchini Uingereza na Ufaransa.
Katika Jumba la Makungusho la Uingereza mjini London vinaoneshwa vitu vyenye thamani elfu makumi kadhaa vilivyochukuliwa kutoka bustani ya Yuanming. Mfalme Napoleon wa tatu wa Ufaransa alijenga 'Jumba la China" katika boma moja maarufu la nchini Ufaransa kwa kuonesha vitu zaidi ya elfu moja vya utamaduni vya China.
Tetesi Kuhusu Visukusuku vya Sokwe-Mtu Wa Beijing
Visukuku vya sokwe-mtu wa Beijing kabla ya kupotea vilihifadhiwa katika sanduku la chuma la usalama la hospitali moja ya mji wa Beijing.
Siku chache kabla ya kuzuka vita ya Pasifiki, profesa Wei Dunrui, ambaye ni mtaalamu mashuhuri wa utafiti wa visukuku hivyo, aliona kuwa hospitali hiyo haikuwa mahali salama tena, hivyo alipendekeza kuvipeleka na kuhifadhiwa visukuku hivyo nchini Marekani. Siku moja ya wiki 2 au 3 kabla ya kuzuka tukio la Pearl Harbor, ofisa wa idara ya huduma ya hospitali hiyo Bo Wen aliarifu kuviweka visukuku 147 yakiwemo mafuvu 5 katika masanduku mawili ya mbao na kuyasafirisha hadi kwenye ubalozi wa Marekani mjini Beijing ili yasafirishwe pamoja na askari wa Marekani hadi Marekani. Lakini tokea hapo visukuku hivyo vilipotea na hakuna habari yoyote kuhusu visukuku hivyo.
Katika miaka ya karibuni, mtaalamu kuhusu elimu ya binadamu Bw. Zhou Guoxing alisikia kuwa siku chache kabla ya kusuka tukio la Pearl Harbor, askari mmoja aliyelinda mlango kati ya makao makuu ya jeshi la baharini la Marekani na ofisi ya ubalozi wa Marekani, aliona watu wawili walikuwa wakibeba sanduku moja na kulifukia katika ua ulioko sehemu ya nyuma ya nyumba ya ofisi ya ubalozi, na alikisia kuwa vitu vilivyokuwemo ndani ya sanduku hilo vilionekea kuwa ni visukuku vya sokwe-mtu wa Beijing. Bw. Zhou Guoxing alifika hapo, lakini hakuweza kuchimba, kwani sehemu hiyo imejengwa nyumba. Visukuku hivyo vilipotea kabla ya miaka miongo kadhaa iliyopita na hakuna habari yoyote kuhusu vitu hivyo. Hayati Zhou Enlai alipokuwa hai aliwahi kusema kuwa ni wachina kadhaa, ambao walikabidhi visukuku vya sokwe-mtu kwa wamarekani na vilipotea mikononi mwa wamarekani, wanasayansi waadilifu wangevirudisha kwa China.
Habari zisizofahamika kuhusu Yang Yuhuan
Yang Yuhuan alikuwa mke mdogo wa mfalme Li Mao ambaye ni mtoto wa mfalme Tang Xuanzong, hapo baadaye alipendwa na Tang Xuanzong na kuwekwa katika jumba la kusini la mfalme. Baadaye Yang Yuhuan alithibitishwa kuwa mke mdogo wa mfalme Tang Xuanzong na kuishi kama malkia. Wakati ule mfalme Tang Xuanzong alikuwa na umri wa miaka 56 na Yang Yuhuan alikuwa na umri wa miaka 22.
Yang Yuhuan alikuwa ni kisura na mnene kiasi, alikuwa anafahamu sana muziki, kucheza ngoma na namna ya kumfurahisha mfalme, hivyo alipendwa sana na mfalme Tang Xuanzong.
Kutokana na Yang Yuhuan kupendwa na mfalme Tang Xuanzong, jamaa zake wote walinufaika sana kutokana naye. Baadhi ya ndugu zake walikuwa maofisa hata mmoja wao alikuwa waziri mkuu ambaye alijitwalia madaraka makubwa. Mfalme alipenda sana wanawake, kunywa pombe na kuponda raha, hatimaye ukatokea "uasi wa Anshi". Mfalme Tang Xuanzong hakuwa na la kufanya ila tu alimtaka Yang Yuhuan ajiue.
Kuhusu kifo cha Yang Yuhuan kuna misemo ya aina nyingi. Baadhi ya watu wanasema kuwa Yang Yuhuan hakufa, mtu aliyekufa ni mwanamke mmoja aliyefanana naye. Mtafiti wa kitabu cha hadithi maarufu cha "Ndoto kwenye Jumba Jekundu" Bw. Yu Pingbo alisema kuwa yule aliyejinyonga alikuwa ni msichana mtumishi wa mfalme, lakini Yang Yuhuan alikimbilia Japan.
Mwaka 1963 kulikuwa na msichana mmoja wa Japan ambaye alionesha nasaba kuhusu ukoo wake na kusema kuwa yeye ni kizazi cha Yang Yuhuan. Nyota wa filamu ya sinema wa Japan msichana Momoe Yamaguchi pia alijidai kuwa ni kizazi cha Yang Yuhuan.
Nchini Japan pia kuna misemo ya aina nyingi. Mmoja wa misemo hiyo unasema kuwa yule aliyekufa alikuwa mwanamke aliyefanana na Yang Yuhuan, lakini Yang Yuhuan mwenyewe alikimbilia kijiji kimoja nchini Japan.
Baada ya kutuliza "uasi wa Anshi" mfalme Tang Xuanzong alituma mtu kwenda Japan kumtafuta Yang Yuhnan, Yang Yuhuan alikabidhiwa sanamu mbili za budhaa alizotoa mfalme Tang Xuanzong, na Yang Yuhuan alitoa pambo moja la kichwani kama zawadi kwa mfalme. Sanamu hizo mbili hadi hivi sasa bado zinahifadhiwa nchini Japan, mahali alipozikwa Yang Yuhuan. Mbele ya kaburi la Yang Yuhuan kuna mbao mbili zenye maelezo, moja ni kuhusu kaburi na nyingine ni kuhusu Yang Yuhuan. Wajapan wanapenda kutoa heshima kwenye kaburi la Yang Yuhuan, wakiona kuwa kufanya hivyo wataweza kuzaa mtoto mzuri. Hivi sasa serikali ya Japan inafikiria kufanya kaburi la Yang Yuhuan kuwa sehemu moja ya utalii kwa watu.
Kaburi la mfalme Qinshihuang
Kaburi la mfalme Qinshihuang liko kwenye tarafa ya Yanzhai, umbali wa kilomita 5 upande wa mashariki wa mji mkuu wa wilaya ya Lintong mkoani Shanxi. Ukiangalia kutoka angani, kaburi hilo linaonekana kama piramidi kubwa. Eneo la kaburi hilo lina kilomita za mraba 66.25, ambalo ni kubwa kwa zaidi ya mara 2 kuliko eneo la mji wa Xian wa hivi sasa.
Tangu aliporithi ufalme alipokuwa na umri wa miaka 13, mfalme Qinshihuang alianza kujijengea kaburi kwenye mlima wa Li, baada ya kuunganisha nchi nyingine 6, alikusanya watu zaidi ya laki moja kutoka sehemu mbalimbali kuendelea kumjengea kaburi, ujenzi uliendelea kwa miaka 37 hadi alipokufa akiwa na umri wa miaka 50.
Kitabu cha historia kinasema kuwa jumba la kuwekea maiti ya mfalme Qinshihuang lilichimbwa chini ya chemchemi na kuimarishwa kwa maji ya madini ya shaba, ndani yake viliwekwa vito na vitu vingine vyenye thamani. Ili kuzuia wezi kuingia ndani ndani ya jumba la kaburi iliwekwa upinde na mishale mingi, ambayo inajirusha yenyewe wakati inapoguswa. Pembeni mwa kaburi ziliwekwa sanamu nyingi za askari na farasi. Usanifu wa kaburi ulizingatia kuonesha madaraka na heshima ya mfalme huyo.
Kutokana na "Kitabu cha Han" na kitabu cha "Maelezo ya Shuijing", kaburi la mfalme Qinshihuang lilitobolewa na Xiang Yu mwaka 206 kabla ya Kristu. Xiang Yu alipeleka askari laki 3 na kusafirisha vitu vilivyokuwemo ndani ya kaburi kwa siku 30.
Lakini wako baadhi ya watu wanaosema kuwa mwandishi maarufu wa "Kitabu cha Historia" aliandika makala maalumu kuhusu mfalme Qinshihuang, lakini hakueleza hata neno moja kuhusu kuharibiwa kwa kaburi la mfale Qinshihuang, lakini mwandishi wa kitabu cha "Maelezo ya Shuijing" aliandika maelezo kamili katika miaka 600 hapo baadaye kuhusu matukio hayo, ambayo yanatia watu mashaka.
Baada ya mwaka 1949, watafiti wa mabaki ya kale wa China walifanya uchunguzi juu ya kaburi la mfalme Qinshihuang, hususan baada ya kugunduliwa kwa sanamu ya askari na farasi. Watafiti hao walitoboa matundu zaidi ya 200, waligundua matundu mawili yaliyochimbwa na wezi, ambayo yalikuwa na kipenyo cha sentimita 90 na urefu wa kwenda chini kwa mita 9, lakini matundu hayo mawili yako kwenye umbali wa mita 250 kutoka sehemu ya katikati ya kaburi, na wote hawakuingia katika jumba lililoko chini ya ardhi. Hivyo, maelezo yaliyoandikwa na Li Daoyuan kuhusu Xiang Yu kuchimba kaburi si ya kweli. Inakisiwa kuwa vitu walivyochukua akina Xiang Yu vilikuwa vitu vilivyoko katika majengo mengine ya kaburi la mfalme Qinshihuang. Kama hali halisi ni kama ilivyokisiwa, basi kaburi la mfalme Qinshihuang litakuwa jumba la kwanza kwa ukubwa duniani lililoko chini ya ardhi.
|