Historia ya China
Habari kuhusu njia ya hariri
Njia ya hariri ni njia muhimu ya kuenea kwa ustaarabu wa kale wa China kwa nchi za magharibi, na ni daraja la maingiliano ya uchumi na utamaduni kati ya China na nchi za magharibi.
Njia ya hariri inaanzia mji wa Changan kwa upande wa mashariki hadi Rome kwa upande wa magharibi, njia hiyo ina matawi mawili, ambayo njia ya kusini omatpla Denghuang kupitia Xinjiang na Afghanistan, Iran, peninsula ya Uarabu hadi nchi ya Rome. Njia ya kaskazini inatoka Denghuang, kupitia sehemu ya Asia ya kati ya Russia kisha inaelekea upande wa kusini magharibi na kuungana na njia ya ile ya kusini. Njia zote mbili zinajulikana kama ni "njia za hariri ardhini".
Aidha, kuna njia mbili za hariri ambazo watu wengi hawazifahamu. Moja ya njia hiyo inajulikana kwa j9na la "njia ya hariri ya kusini magharibi". Njia hiyo inatoka mkoa wa Sichuan, kupitia mto wa Yiluowadi, Menggong iliyoko sehemu ya kaskazini ya nchi ya Myanmarr, baada ya kuvuka mto wa Qindun, inafikia Nepal iliyoko sehemu ya kaskaizni mashariki ya India, kisha inafuata mto wa Ganges, kisha inapitia sehemu ya kaskazini magharibi ya India na kufika kwenye uwanda wa juu wa Iran. Njia hiyo ya hariri ilikuweko mapema zaidi kuliko zile za ardhini.
Njia nyingine ya hariri inatoaka mji wa Guangzhou, kupitia mlango bahari wa Malacca, Sri lanka, India hadi Afrika ya mashariki. Njia hiyo inajulikana kwa "njia ya hariri ya baharini". Mabaki ya kale yaliyofukuliwa kutoka baadhi ya sehemu za Afrika mashariki ikiwemo Somalia, yanathibitisha kuwa njia hiyo ya hariri ilianzishwa katika enzi ya Song ya China.
"Njia ya hariri ya baharini" iliunganisha nchi muhimu za asili ya ustaarabu na sehemu za chanzo cha utamaduni duniani, ambazo zinahimiza maingiliano ya uchumi na utamaduni ya katika sehemu hizo, hivyo inaitawa kuwa ni "njia ya mazungumzo kati ya mashariki na magharibi. Kitabu cha historia kinasema kuwa msafiri Maco Polo hapo zamani alifika China kwa kupitia "Njia ya hariri ya baharini". Wakati aliporejea nyumbani pia alipanda marikebu kutoka Quanzhou ya mkoa wa Fujian na kuridi Venice, Italia.
Kuhusu Jina la Ngome ya Ukuta Mkuu
Sehemu zote muhimu za ukuta mkuu zilijengwa ngome kupatiwa majina kwa ngome hizo ni kwa kujifurahisha.
Ngome ya Shanhai, ambayo ina maana ya mlima na bahari katika lugha ya kichina, inajulikana kuwa ni ngome ya kwanza ya ukuta mkuu. Ngome hiyo iko kwenye mpaka kati ya mikoa ya Hebei na Liaoning na ni mwanzo wa ukuta mkuu. Ngome ya Shanhai iko karibu na mlima wa Yan na bahari ya Bo. Mtu akipanda kwenye ngome hiyo anaburudishwa sana na mandhari nzuri ya mlima na bahari, hivyo ngome hiyo ilipewa jina la mlima na bahari.
Mwanzo wa ukuta mkuu katika upande wa magharibi ni ngome ya Jiayu kwenye mji wa Jiayu mkoani Gansu. Ngome hiyo ilijengwa katika mwaka 1372 wa enzi ya Ming. Ngome hiyo ilipewa jina hilo kutokana na kutokana na kujengwa kwake kwenye mlima wa Jiayu. Hapo baadaye ngome hiyo ilijulikana kama ngome ya amani kutokana na kutokuwa na vita kwenye sehemu hiyo.
Kuhusu Majina ya Mahali Kisiwani Taiwan
Katika historia, Taiwan iliwahi kuitwa kuwa Yizhou, Dongfan na Dayuan. Hapo baadaye watu waliita Taiwan kuwa "Kisiwa cha Hazina" kutokana na kuwa na rasilimali nyingi, "Kisiwa cha matufaha pori ya kichina" (umbo lake linafanana na majani yake), "Kisiwa cha Spring" (hali ya hewa yake si joto wala baridi), "Kisiwa cha Vipepeo" (kuna vipepeo wengi), kisiwa cha marijani (kuna marijani nyingi), na "Kisiwa cha Sukari" (kuna miwa mingi). Wakoloni wa Ulaya waliwahi kuita Taiwan kuwa "Farmosa" (Kisiwa Kizuri), vilevile waliwahi kuita Taiwan kuwa "Kisiwa cha Wavuvi".
Kwa Nini Wachina Wanaitwa "Vizazi Vya Dragon"
Wachina wanaitwa kuwa "vizazi vya dragon", chanzo chake ni alama na hadithi ya kale. Inasemekana kuwa kabla ya mfalme Huang kulishinda kabila la Ciyou na kuunganisha sehemu za kati za China alichukulia "dubu" kama ni alama yao, lakini baada ya kuliteka kabila la Ciyou ili kufariji maeneo yaliyojisalimisha mfalme Huang aliacha kutumia alama hiyo ya "dubu" na kutumia "dragon" kama ni alama yao mpya, ambayo ni mchanganiko wa kichwa cha "dubu" na mwili wa aina moja ya "nyoka". Alama ya "dragon" ni mchanganiko wa taswira za jamii za wanaume na wanawake, hali ambayo inaonesha historia ya maendeleo ya taifa na mchakato wa muungano wa makabila mbalimbali ya China.
"Dragon" ikawa alama ya babu za jadi za taifa la China, hivyo taifa la China limehusishwa na "dragon". Kulikuwa na hadithi inayosema kuwa mfalme Yan ni mtoto wa mwanamke aliyejulikana kwa jina la "Deng" kutokana na kuhurumiwa na mungu wa Dragon wa mbinguni. Maadamu babu jadi wa taifa la China alikuwa kizazi cha "Dragon" wa mbinguni, hivyo vizazi vya taifa la China vilevile ni vizazi vya dragon.
Utamaduni wa Majina wa China
Kila mtu anapewa jina tangu anapozaliwa, na baadaye atashiriki katika shughuli za jamii kwa kutumia jina lake, ambalo linafanya kazi ya kumwakilisha na kumtofautisha na watu wengine. Lakini katika jamii ya China ya kale, majina yana maana kubwa zaidi.
Katika historia ndefu, utamaduni wa majina ya wachina ulikuwa kitu muhimu katika maisha halisi na maisha ya kiroho ya taifa la China, na ulifanya kazi muhimu katika maeneo ya saisa, utamaduni na jamii. Data za utafiti wa mabaki ya kale zinaonesha kuwa zaidi ya miaka milioni moja iliyopita, wachina walikuwa wameishi katika ardhi ya nchi hiyo ya kale, lakini historia ya "majina" ilianza katika jamii ya kiume ya miaka 5,000 au 6,000 iliyopita. Umaalumu wa jamii ya kike ni kuwa wanawake walikuwa na hadhi ya kuongoza katika usimamizi wa shughuli za ndani za jamii, na kufuata utaratibu wa kuoana kati ya koo tofauti, ambapo watu wa ukoo mmoja ilikuwa ni mwiko kuoana. Kwa kufuata utaratibu huo, kulikuwa na haja ya kuchunguza uhusiano wa watu wa kila jamii, hivyo yakatokea majina ya koo ili kuthibitisha uhusiano wa damu moja.
Utafiti uliofanywa na Gu Yanwu, mwanachuo mashuhuri wa enzi ya Qing unaonesha kuwa zamani za kale nchini China kulikuwa na majina ya koo 22, na huenda kulikuwa na majina mengi zaidi ya koo, lakini huenda yalizama katika maji ya mto wa historia, na yale yaliyoendelea pia yalikuwa na mabadiliko makubwa. Kabla ya miaka 4,000 au 5,000 iliyopita, baada ya kupita katika jamii ya kike, wachina waliingia katika kipindi cha jamii ya kiume, jamii yenye koo mbalimbali iliingia haraka katika jamii yenye matabaka ya watu. Moja ya alama muhimu za kipindi hicho cha mpito ni kuingiliana na kupigana kati ya koo zenye mababu jadi mbalimbali.
Katika karne ya 3 kabla ya Kristu, enzi ya Qin iliunganisha sehemu zote za China, ambapo majina ya koo yaliyotoka katika jamii ya kike mwanzoni kabisa yaliungana na majina ya koo yaliyotoka katika jamii ya kiume. Tokea hapo katika jamii ya umwinyi iliyoendelea kwa miaka zaidi ya 2,000, enzi zilibadilishwa kwa miongo kadhaa, na kila badiliko lilipotokea hutokea maeneo ya ardhi ya tuzo na kutokea majina mapya ya koo. Utamaduni wa namna hiyo ulirithiwa na vizazi vya baadaye. Wazo kali la kufuatilia majina ya koo za babu jadi ni kiini cha umoja huo. Hadi hivi sasa bado kuna wachina wanaoishi nchi za nje ambao wanarejea China kufuatilia vyanzo vya koo zao.
Jinsi Utaalamu wa Ufunguji wa Mafunza wa Hariri Ulivyoenezwa Kwenye Nchi za Magharibi
Inasemekana kuwa malkia Luo mke wa mfalme Huang aliwafundisha watu utaalam wa ufugaji wa mafunza wa hariri miaka zaidi ya 5,000 iliyopita.
Katika enzi ya Han ya magharibi, Zhang Qian alisafiri kwa upande wa magharibi na kupeleka vitambaa vya hariri hadi Ulaya. Watu wa Ulaya walipoona vitambaa laini na vya kung'ara walivinunua haraka.
Mwanzoni watu wa Ulaya hawakujua vitambaa hivyo vilifumwa kwa nyuzi zilizotolewa na mafunza wa hariri, walifikiri kuwa nyuzi hizo zilitolewa katika mti fulani, kisha kulainishwa kwa maji. Baada ya kujua kuwa vitamba hivyo vilifumwa kutokana na nyuzi za mafunza wa hariri, walipania kujifunza utaalam wa kufuga mafunza wa hariri.
Ilipofika karne ya 6, mfalme Jadincean wa Rome alionana na padri mmoja aliyewahi kufika China na kumtaka aende China kuiba mbinu ya kufuga mafunza wa hariri. Padri huyo alifika Yunnan, China alifahamishwa maarifa ya kufuga mafunza wa hariri kwa majani ya miforosadi, alirejea Rome kwa haraka, lakini alikanganyika badala ya kupasha joto mbegu wa mafunza kifuani mwake alizipanda kwenye ardhi na kuweka mbegu wa mti wa mforosadi kifuani mwake badala ya kuzipanda kwenye ardhi, hatimaye alishindwa. Padri huyo alituma mapadri wengine wawili waende China kukamilisha kazi hiyo, mapadri hao wawili walikumbuka sana fundisho alilopata yule padri wa kwanza na kuweka maandishi kuhusu upandaji miti na kupasha joto mbegu za mafunza wa hariri katika uwazi wa katikati ya bakora zao na kurudi Rome. Tokea hapo maarifa ya ufugaji wa mafunza wa hariri yaliingia barani Ulaya.
Asili na Mabadiliko ya Maneno ya Kihan
Maneno ya kabila la wahan ni moja ya maneno yaliyotumika kwa miaka mingi, yenye nafasi kubwa ya matumizi na kutumiwa na idadi kubwa sana ya watu duniani. Kuvumbuliwa na kutumika kwa maneno ya kihan, si kama tu kumehimiza maendeleo ya utamaduni wa taifa la China bali pia kumeathiri sana maendeleo ya utamaduni wa dunia.
Zaidi ya miaka 6,000 iliyopita kwenye sehemu yalipo majengo ya Banpo, kulikuwa na aina zaidi ya 50 za michoro, inayoonekana kama ni maandishi ya kawaida, wataalamu wanasema kuwa huenda hiyo ndiyo asili ya maneno ya kihan.
Maneno ya kihan yalikamilika katika hatua ya mwanzo katika enzi ya Shang karne ya 16 kabla ya Kristu. Katika kipindi cha awali cha enzi ya Sahng, ustaarabu wa China ulifikia kiwango cha juu, na moja ya alama yake ni kuwa na maandishi yaliyochungwa kwenye magamba ya kobe. Katika enzi ya Sahng, mfalme kabla ya kufanya jambo lolote alikuwa huagua, kwa kutumia mabamba ya kobe.
Hivi sasa watafiti wa mabaki ya kale wamegundua mabamba ya kobe vipande zaidi ya elfu 160 vyenye maneno zaidi ya 4,000. Maandiko kwenye magamba ya kobe yalikuwa msingi wa maendeleo ya maneno ya kabila la wahan.
Maandiko ya maneno ya kihan, ambayo yanafanana na vitu vyenyewe, yana maneno kiasi cha elfu 10 na yale yanayotumika mara kwa mara ni kiasi cha elfu 3.
Kuvumbuliwa maneno ya kihan kulileta athari kubwa kwa nchi jirani. Maandiko ya kijapan, kivietnam na kikorea yalivumbuliwa kwa msingi wa maneno ya kihan.
Sauti ya Kongele la Yongle Zafikia Umbali wa Kilomita 45
Katika hekalu ya Dazhong mjini Beijing kuna kengele moja kubwa inayojulikana kwa jina la dazhong. Kengele hiyo, ambayo ilitengenezwa miaka zaidi ya 500 iliyopita, ina uzito wa tani 46.5, kimo cha mita 6.75 na kipenyo cha mita 3.3.
Sauti ya kengele ya Yongle ni nzuri sana, mawimbi ya sauti yake yanalingana na mawimbi ya sanifu ya muziki. Kangele hiyo inapogongwa taratibu, sauti yake ni ndogo na inavutia, na inapogongwa kwa nguvu sauti yake ni kubwa na nene, ambayo inaweza kufikia umbali wa kilomita 45 na sauti hiyo inaendelea kwa dakika zaidi ya 2.
Kila ifikapo siku ya mwaka mpya, kengele kubwa ya Yongle hugongwa, na desturi hiyo imeendelea kwa miaka zaidi ya 500. Wataalamu wa China walifanya upimaji kuhusu kengele hiyo, waliona kuwa kengele hiyo ilitengenezwa kwa madini za shaba, bati, lead, chuma na magnesium,licha ya madini hayo, ndani yake kuna dhahabu na fedha ambazo uzito wake ni kilo 18.6 na kilo 38.
Mtaalamu mmoja husika alisema kuwa kengele hiyo ni ajabu duniani katika sekta ya kusubu, utengenezaji wake ni kazi ngumu hata hivi sasa.
Maajabu Yaliyogunduliwa kwa "Remote Sensing"
Katika miaka ya karibuni wataalamu walipiga picha ya mji wa Beijing kutoka angani kwa teknolojia ya "remote sensing", waliwaona dragon wawili waliolala na jitu mmoja lililo keti kwenye eneo la mji, hayo yamekuwa maajabu mawili ya mji wa Beijing.
Picha ya rangi iliyotokana na teknolojia hiyo inaonesha kuwa dragon wa kwanza anaundwa na majengo ya kale ya Beijing kuanzia jengo la Tiananmen hadi jengo la Zhonggu. Na dragon mwingine anaundwa na mito na mifereji ya Beijing na kujulikana kwa "dragon wa maji".
Ajabu lingine la Beijing ni taswira ya bustani ya Jingshan ambayo inaonekana kama jitu moja lililokaa chini. Bustani ya Jingshan ilikuwa ya wafalme na iko katika upande wa kaskazini mwa majumba ya wafalme wa zamani. Je hali hiyo ni inatokana na kusanifiwa au ilitokea kwa bahati tu? Hilo ni swali ambalo mpaka sasa halijajibiwa.
Sindano ya Mfupa na Mapambao ya Sokwe-Mtu
Katika kipindi cha zama mawe cha zamani kiasi cha miaka elfu 50 iliyopita, binadamu walijua kutengeneza na kutumia sindano. Sindano hiyo ilitengenezwa kwa mfupa. Watafiti waliwahi kugundua sindano ya mfupa huko Ozuina barani Ulaya, lakini sindano ile ilitengenezwa kwa ufundi wa kiwango cha chini sana. Sindano iliyogunduliwa katika pango waliloishi sokwe-mtu ilitengenezwa kwa ufundi mkubwa zaidi.
Sindano hiyo ina urefu wa milimita 82 na unene wa milimita 3, ambayo inafanana na njiti ya kiberiti, sindano hiyo ni laini na yenye ncha kali. Watafiti wanasema kuwa sindano hiyo inatufahamisha kuwa, wahenga walioishi mapangoni walikuwa wanavaa nguo.
Wahenga hao walikuwa wanaishi kwenye mapango milimani miaka zaidi ya elfu 18 iliyopita, walijua kutengeneza na kuvaa vitu vya mapambo. Watafiti waligundua mkufu uliotengenezwa kwa mawe, meno ya wanyama, mfupa wa samaki na simbi za baharini.
|