18: Mila na Desturi

Desturi wakati wa Sikukuu

Siku kuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina

Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina ni sikukuu kubwa kabisa kwa Wachina katika mwaka mzima ambayo ni kama sikukuu ya Krismasi katika nchi za Magharibi. Ingawa namna ya kusherehekea sikukuu hiyo inabadilika badilika kutokana na jinsi muda unavyokwenda, lakini nafasi muhimu ya sikukuu hiyo katika maisha ya Wachina haitabadilika kabisa. Yafuatano ni maelezo kuhusu sikukuu hiyo.

Inasemekana kuwa hadi sasa Sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina imekuwa ikiadhimishwa kwa miaka elfu nne nchini China, lakini mwanzoni sikukuu hiyo haikuitwa sikukuu ya Spring na wala haikuwa na tarehe maalumu. Hadi miaka elfu mbili na mia moja iliyopita wahenga wa China walihesabu mwaka kwa mzunguko kamili wa sayari ya Jupita, sikukuu hiyo iliitwa sikukuu ya Jupita, ilipofika miaka elfu moja iliyopita ndipo Wachina walipoanza kuiita siku hiyo sikukuu ya Spring.

Kutokana na desturi ya Wachina sikukuu hiyo inaanzia tarehe 23 mwezi wa 12 kwa kalenda ya Kichina hadi tarehe 15 mwezi wa Januari yaani kuwadia kwa sikukuu ya taa, ambapo ni jumla ya wiki tatu. Katika siku hizo za mwaka mpya, siku ya mwisho yaani tarehe 30 ya mkesha wa sikukuu na siku ya kwanza ya Januari ni siku za sherehe, au kwa maneno mengine siku hizi mbili ni kilele cha sikukuu ya Spring.

Ili kusherehekea sikukuu ya Spring, kuanzia mijini hadi vijijini watu huwa katika pilikapilika za matayarisho. Huko vijijini wakulima hufanya usafi wa nyumba, kufua nguo, kubandika mlangoni karatasi pacha zenye maandishi ya baraka na kubandika picha maalumu za mwaka mpya vyumbani, huku wakitayarisha mahitaji ya mwaka mpya kwa kununua keki, peremende, nyama, vinywaji na matunda ili kutumia nyumbani na kukaribisha wageni. Katika miji maandalizi ya mwaka mpya yanaanza mapema zaidi, maduka na masoko ya kujihudumia hutayarisha vitu tele. Kutokana na takwimu, Wachina hutumia pesa kiasi cha thethuli moja au pengine hata zaidi ya matumizi yote ya mwaka mzima katika kipindi cha sikukuu ya Spring.

"Kukesha usiku" wa kuamkia sikukuu ya Spring ni desturi ya Wachina, kwa kawaida katika usiku huo jamaa hukusanyika pamoja kwenye chakula, hali ambayo inaonekana kote iwe ni sehemu ya kaskazini au kusini ya China. Jamaa hula chakula kwa pamoja, na baada ya chakula huburudika hadi mapambazuko. Katika usiku huo wazee huwazawadia watoto pesa kama ishara ya baraka kwa mwaka unaokuja. Katika miaka kadhaa iliyopita watu walisherehekea sikukuu hiyo kwa kuwasha fataki ikimaanisha kuwafukuza mashetani, lakini kutokana na usalama na uchafuzi wa mazingira desturi hiyo imepigwa marufuku katikati ya miji mikubwa.

Wakati wa sikukuu halisi yaani siku ya kwanza ya mwezi wa kwanza watu huvalia rasmi wakisubiri kutembelewa na wageni au kutoka kwenda kuwatembelea jamaa na marafiki. Wanapokutana huamkiana "Heri ya Mwaka Mpya", au "Heri ya Sikukuu ya Spring" na kuwakaribisha ndani kwa peremende, chai na vitafunwa na kuzungumzia maisha yao ya kila siku. Kama majirani walikuwa na mkwaruzano katika mwaka uliopita, wanapaswa kuondoa kinyongo na kutembeleana katika sikukuu.

Wakati wa sikukuu ya Mwaka mpya wa jadi wa kichina, idara za utamaduni hushirikisha michezo ya sanaa ya aina mbalimbali. Kwa mfano, usiku wa mkesha vituo vya televisheni huonyesha sherehe maalumu ya michezo toka saa mbili za usiku hadi saa saba usiku, ambapo huwepo watazamaji zaidi ya milioni mia moja. Licha ya michezo ya Wachina pia kuna vikundi vya sanaa kutoka nchi nyingine kama Russia, Uingereza na Marekani vikifanya maonesho ya muziki au dansi.

Shamrashamra za sikukuu pia zinafanyika katika bustani, ambapo kwamba kuna magulio, michezo ya mazingaombwe n.k.

Kutokana na mabadiliko ya maisha, watu wameanza kutumia simu za waya, simu za mkononi, na hata mtandao wa kompyuta kupelekeana salamu.

Siku ya Tarehe 7 ya mwezi wa 7 kwa kalenda ya kilimo ya China yaani sikukuu ya kuomba baraka

Tarehe 7 ya mwezi wa 7 kwa kalaenda ya kilimo ya China ni siku ya kuomba baraka kwa wananchi wa China, inasemekana kuwa, siku hiyo pia ni siku ya kukutana kwa nyota ya Niu Lang na nyota ya Zhi Nu.

Hadithi ilisimulia kuwa, katika zama za kale sana, mbingu ilikuwa ni ya buluu tupu, kulikuwa hakuna mawingu hata kidogo. Mfalme wa mbingu aliona kuwa mbingu na rangi ya buluu peke yake si wa kupendeza, hivyo aliwaambia binti zake 7 wasokote nyuzi na kufuma vitambaa ili kuishonea nguo "mbingu". Lakini vitambaa vilivyofumwa na binti zake 7 vyote vilikuwa vya rangi ya kijivujivu au nyeupe, vilikuwa bado havipendezi. Binti wa 7 ambaye ni binti mdogo kabisa lakini ni mwenye akili nyingi. Siku moja aligundua maua ya aina moja yaliyochanua yana rangi ya aina 7, kwa hivyo alichuma maua hayo mengi na kupaka rangi mbalimbali kwenye nyuzi walizosokota, baada ya juhudi zake, binti zao walifaulu kufuma vitambaa vyenye rangi mbalimbali, walifurahi sana na dada huyo mdogo alisifiwa kuwa ni binti mwerevu, ambapo waliamua kwa kauli moja kuwa, katika siku za kawaida, wataivalisha "mbingu" nguo nyeupe; siku ya mvua, wataivalisha nguo ya kijivu; na asubuhi na jioni wataivalisha nguo za rangi. Mfalme wa mbinguni alipoambiwa, alifurahi sana, akampa binti yake mdogo hadhi ya malaika "Zhi Nu."

Malaika Zhi Nu kila siku alifuma vitambaa, akijisikia uchovu, huangalia mandhari ya dunia chini ya mbingu. Kijana mmoja aliyefuga ng'ombe alivutiwa macho, aliona kijana huyo kila siku alilima shamba peke yake, alipopumzika, aliongea tu na ng'ombe aliyemfuga, Zhi Nu alimhurumia sana. Kijana huyo aliitwa Niu Lang.

Siku moja ng'ombe mzee alimwambia Niu Lang: "Kesho ni tarehe 7 Julai, binti 7 wa mfalme wa mbinguni watafika duniani kuoga. Ukificha nguo ya malaika Zhi Nu, atakuwa mke wako." Niu Lang aliamua kwenda kujaribu.

Siku hiyo tarehe 7 Julai, Niu Lang alijificha ndani ya matete kando ya mto, muda si mrefu baadaye, aliona malaika 7 waliosimama juu ya mawingu 7 wakija duniani, wakifika kando ya mto wakivua nguo zao, wakajitupa ndani ya maji kuogelea. Papo hapo Niu Lang akachukua nguo ya malaika Zhi Niu, halafu akakimbia kwa haraka, vishindo vya matete viliwashtusha malaika 7, wakajiondoa kutoka mto, malaika 6 wakavaa nguo zao na kuruka mbinguni, ila tu malaika Zhi Niu hakuona nguo zake zilipo, akahangaika sana na kusimama kwenye kando ya mto. Niu Lang akamwomba malaika Zhi Niu kuwa, kama akikubali kuolewa naye, atampa nguo yake. Malaika Zhi Niu alipoona Niu Lang ndiye kijana yule anayempenda, alikubali kwa haya kuolewa na Niu Lang.

Jioni ya siku hiyo, Niu Lang na Zhi Nu wakafunga ndoa chini ya usimamizi wa ng'ombe mzee. Katika miaka miwili baadaye, mfumaji nguo alizaa mvulana mmoja na msichana mmoja. Mume na mke, mmoja alilima shamba, mwingne alifuma nguo, maisha yao yalikuwa ni mazuri sana.

Baada ya miaka kadhaa kupita, walijaliwa watoto wawili, wa kiume na wa kike, na hivyo furaha ilitawala familia hiyo.

Lakini siku moja ghafla mawingu mazito yalitanda mbinguni, kimbunga kilivuma kwa nguvu, na askari wawili wa mbinguni wakashuka kwenye nyumbani kwao. Niu Lang akaambiwa kwamba Zhi Nu alikuwa mtoto wa mfalme wa mbinguni, amekuwa akitafutwa kwa miaka kadhaa iliyopita. Askari walimrudisha Zhi Nu mbinguni kwa nguvu.

Niu Lang akiwa na watoto wawili kifuani alibaki kumwangalia mkewe akichukuliwa na askari wawili kurudi mbinguni, alihuzunika sana, lakini aliapa kwamba atakwenda mbinguni kumchukua mkewe Zhi Nu ili kukamilisha familia yake. Lakini binadamu atawezaje kufika mbinguni?

Niu Lang alipoishiwa na ujanja, ng'ombe wake mzee alimwambia, "Nichinje mimi na kujifunika ngozi yangu mgongoni; kwa namna hiyo utaweza kuruka kwenda mbinguni." Niu Lang kamwe hakukubali, lakini ng'ombe alishikilia. Kwa kuona hana njia nyingine Niu Lang alimchinja huku akilia.

Niu Lang alijifunika kwa ngozi ya ng'ombe, akawabeba watoto wawili kwa mzegazega, mmoja mbele, mmoja nyuma, akaruka kwenda mbinguni. Lakini huko kwenye kasri ya mbinguni watu waligawanyika kwa matabaka, hakuna yeyote aliyemheshimu kabwela maskini na hohe hahe kama Niu Lang. Mungu alimkatalia ombi lake la kuonana na mkewe Zhi Nu.

Niu Lang na watoto wake walimsihi sana, mwishowe aliruhusiwa kumwona mkewe kwa muda mfupi. Mkewe Zhi Nu aliyekuwa amefungwa alipowaona mumewe na watoto wake alijawa na furaha na huzuni. Kufumba na kufumbua muda ukapita, mungu akaamuru kuondolewa kwa Zhi Nu. Maskini Niu Lang na watoto wake walimkimbilia kadri wawezavyo huku wakianguka anguka na kuinuka. Mwishowe walipomkaribia, mke wa mungu alichomoa kibanio cha nywele akachora mstari angani, na mara mto wa kilimia ukatokea kati yao. Tokea hapo Niu Lang na Zhi Nu wakawa wametenganishwa na mto huo, isipokuwa tu kila tarehe 7 ya mwezi wa 7 wanaruhusiwa kukutana. Kila ifikapo siku hiyo, ndege wasio na idadi waliungana pamoja na kuwa kama daraja juu ya mto huo ili Niu Lang na Zhi Nu wakutane. Katika siku za baadaye, kila ifikapo tarehe 7 mwezi wa 7 kwa kalenda ya kilimo, wasichana huomba baraka kutoka kwa Malaika Zhi Nu, wakichukua sindano 7 na nyuzi za hariri, kama nyuzi zinaweza kupita katundu ya sindano bila kikwazo, hali hii inaonesha kuwa wasichana hao ni werevu. Inasemekana kuwa, usiku wa siku hiyo, watoto wengi hukaa chini ya mizabibu, wakasikia Niu Lang na Zhi Nu wakiongea kwa furaha.

Siku ya Tarehe 9 ya mwezi wa 9 kwa kalenda ya kilimo ya China yaani sikukuu ya Chongyang

Siku hiyo ni siku muhimu ya jadi ya China kwa wananchi wa China. Kila ifikapo siku hiyo, wachina wa familia moja moja wazee na watoto huenda kupanda milima na kuchuma matunda ya cornus na kula keki za maua waliotengeza wenyewe.

Wachina wa zama za kale waliona kuwa, tarakimu 9 ni ishara ya baraka, na tarehe 9 mwezi wa 9 ni siku inayoweza kuleta baraka mara dufu. Inasemekana kuwa, katika karne ya 3 kabla ya kuzaliwa kwa Kristo, alikuwepo mtu mmoja aliyeitwa Fei Changfang, ambaye si kama tu alikuwa na uwezo wa kudhibiti upepo na mvua, pia aliweza kutuma malaika na kukamata mashetani. Kijana mmoja aliyeitwa Huan Jing alimheshimu sana Fei Changfang, alitaka kuwa mwanafunzi wake. Kutokana na nia yake imara, Fei Changfang alimchukua kuwa mwanafunzi wake, na kumfundisha mambo mbalimbali. Siku moja Fei Changfang alimwambia Huan Jing: "Tarehe 9 mwezi wa 9, familia yenu itakumbwa na msiba, kwa hiyo unapaswa kujiandaa kukabiliana na msiba huo." Huan Jing aliposikia alihangaika sana, akapiga magoti mbele ya mwalimu wake akaomba amfundishe mbinu za kukwepa msiba. Fei Changfang alimwambia: "Siku hiyo ya tarehe 9 mwezi wa 9, ungeshona mikoba mingi myekundu na kuweka matunda ya cornus officinalis ndani, halafu weka kwenye mkono wako, uchukue pombe iliyowahi kutiwa maua ya chrysathemum , halafu watu wa familia yenu nzima muende kwenye mteremko wa mlima kunywa pombe, ndivyo hivyo mtakwepa msiba. Ilipofika tarehe 9 mwezi 9 kwa kalenda ya kilimo, Huan Jing na watu wa familia yake walikwenda kwenye mteremko kukaa na kunywa pombe kwa siku moja. Usiku waliporudi nyumbani kwao, waliona kuwa, mifugo waliyofuga nyumbani wote walikufa, kweli walikwepa balaa. Tangu hapo, kila ifikapo siku hiyo, wachina hupanda milima, kuchuma madunda ya cornus na kunywa pombe iliyowahi kutiwa maua ya chrysathemum , desturi hizo ziliendelea kwa zaidi ya miaka 2000.

Shairi moja lililoandikwa na mshairi maarufu sana wa Enzi ya Tang ya China ya kale Wang Wei lilionesha vilivyo desturi za sikukuu ya Chongyang. Shairi lake linasema: "Naishi nje ya maskani yangu, kila ifikapo sikukuu nawafikiria zaidi jamaa zangu. Naona ndugu zangu wote wakipanda mlima na kuchuma matunda ya cornus, nasikitika peke yangu niko nje na kuwakumbuka."

Desturi nyingine ya sikukuu hiyo ni kula keki zilizotengenezwa kwa mchele, na tende, na kuweka bendera ndogo za rangi popote, hivyo keki hiyo iliitwa kuwa keki ya maua. Wakazi walioishi kwenye tambarare wakila keki hiyo, inamaanisha kuwa waliwahi kupanda milima, kwani keki ya kichina tamshi lake la kichina ni Gao, tamshi hilo ni sawasawa na tamshi la Gao nyingine yaani urefu wa mlima, hivyo watu wakila keki walijihisi kama waliwahi kupanda mlima.

Aidha sikukuu hiyo inoonesha maana ya "kuishi maisha marefu". Kwani wachina waliona kuwa desturi za sikukuu hiyo zinaweza kuwawezesha watu waishi maisha marefu. Hivi sasa wachina wanaendelea kudumisha desturia ya kupanda milima na kuchuma matunda ya cornus officinalis , hata dukani siku hiyo huuza keki za maua. Na miaka ya hivi karibuni, wachina waliona siku hiyo tarehe 9 mwezi wa 9, tamshi la 9 la kichina ni Jiu, tarehe 9 mwezi wa 9, kuna 9 mbili, tamshi lake ni sawasawa na neno la kichina Daima milele yaani Jiujiu, hivyo wachina waliamua siku hiyo kuwa ni siku ya wazee, maana ya sikukuu hiyo imeonesha wachina wanaoheshimu wazee, kuwapenda wazee na kuwatakia wazee waishi maisha marefu.

Siku ya Tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo yaani sikukuu ya Duanwu

Tarehe 5 mwezi Mei kwa kalenda ya kilimo ni sikukuu ya Duanwu, sikukuu hiyo na sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina pamoja na sikukuu ya Tarehe 15 mwezi wa 8 kwa kalenda ya kilimo ni sikukuu ya tatu muhimu kwa wachina.

Maana ya kichina ya "Duanwu" ni kuwa, "Duan" ni "Mwanzo", kwa kufuata kanuni za kalenda ya kilimo ya kichina, tarehe 5 mwezi wa 5 ndiyo "Duanwu".

Kuhusu chanzo cha sikukuu ya Duanwu, kuna ufafanuzi mwingi, baadhi ya watu wanaona kuwa sikukuu hiyo ilitokana na desturi za zama za kale za China, kila ifikapo majira ya siku za joto, na wengine walisema kuwa sikukuu hiyo inatokana na watu walioishi kwenye eneo la mtiririko wa Mto Changjiang walioabudu Dragong, lakini wachina wengi waliona kuwa sikukuu hiyo ilitokana na kumbukumbu za watu kwa mshairi mzalendo wa zama za kale Qu Yuan. Qu Yuan aliishi katika Dola la Chu katika karne ya 3 kabla ya Kristo, taifa lake liliposhambuliwa na maaduia kutoka nchi nyingine, alijitupa katika mto Guluojiang akiwa na huzuni kubwa, siku hiyo ilikuwa tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo ya kichina. Tangu hapo kila ifikapo siku hiyo, watu huchukua vyombo vya mianzi kuweka wali ndani na kuvitupa ndani ya mto kwa kumkumbuka Qu Yuan, baadaye wakatengeneza chakula cha Zongzi na kukitupa ndani ya mto.

Kula chakula cha Zongzi ni desturi muhimu katika sikukuu hiyo, Zongzi hutengenezwa kwa majani ya matete au majani ya mianzi, ndani huwekwa wali na hufungwa kwa nyuzi kuwa na umbo la sambusa, na kukichemsha hadi kiive. Kila ifikapo sikukuu hiyo, wachina hutengeneza chakula cha Zongzi na kukichukua kama zawadi kwa jamaa na marafiki.

Mbali ya Zongzi, katika sikukuu hiyo watu hula mayai ya bata yaliyowahi kutiwa chumvi na kunywa pombe ya kimanjano iliyotengenezwa kwa mchele, inasemekana kuwa kufanya hivyo watu wanaweza kukwepa mashetani.

Aidha, sikukuu hiyo pia kuwa desturia maalum ya kuchuma nyasi za wormwood kuzitundika kwenye mlango, nyasi hizo ni dawa ya mitishamba ambayo inaweza kufukuza wadudu wenye sumu. Kwani kila ifikapo sikukuu hiyo ya tarehe 5 mwezi wa 5 kwa kalenda ya kilimo yaani mwanzoni mwa majira ya siku za joto, mvua hunyesha sana, kuna kuwa unyevunyevu mwingi, na wadudu wenye sumu huzaliana wakati huo, ambapo ni rahisi kwa watu kupatwa na maradhi, na mitishamba hiyo inaweza kuwasaidia watu kukinga na kutibu maradhi. Na mpaka sasa, kila ifikapo sikukuu hiyo, wakazi wa vijijini wanashikilia desturi za kuwashonea watoto wao viatu vyenye sura kama chui, kwa maana ya kuwatakia watoto wao baraka. Katika sehemu ya eneo la katikati na la chini la Mto Changjiang, kusini mwa China, desturi muhimu ni kufanya mashindano ya kupiga makasia kwenye mashua. Inasemekana kuwa desturi hiyo ilihusiana na wenyeji wa huko kumkumbuka mshairi mashuhuri Qu Yuan, wenyeji wa huko walipoona Qu Yuan amejitupa ndani ya mto, walipiga makasia mashua kwa haraka wakitaka kumwookoa. Baadaye kitendo hicho kilikuwa desturia ya kufanya mashindano ya kupiga makasia mashua.

Sikukuu ya Taa ya Tarehe 15 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo

Katika kalenda ya Kilimo ya China, tarehe 15 mwezi wa kwanza ni "Sikukuu ya Taa" ya Kichina. Hiyo ni miongoni mwa sikukuu kubwa za Kichina.

Wachina walianza kusherehekea sikukuu hiyo tangu Enzi ya Han, yaani zaidi ya miaka elfu mbili iliyopita. Mfalme Han Wendi alikuwa mfalme wa tatu wa Enzi ya Han baada ya kumpindua mfalme wa pili Lu Hou. Alikalia kiti cha ufalme tarehe ya 15 Januari kwa kalenda ya Kichina. Ili kuikumbuka siku hiyo ya kuwa mfalme, kila mwaka katika siku hiyo mfalme Han Wendi alijifanya raia na kutembelea mjini "kuburudika pamoja na raia" wake. Ingawa simulizi hiyo haijabainika, lakini ni ukweli ni kwamba tangu Enzi ya Han siku hiyo imekuwa siku ya kumtambikia mungu ili kupata baraka.

Binadamu walianza kutumia moto na taa sawia katika maisha yao. Simulizi kuhusu chanzo cha sikukuu ya taa iliyoenea zaidi ni kama ifuatayo:

Katika Enzi ya Han alikuwepo mtu mmoja, aliyeitwa Dong Fangshuo, alikuwa mcheshi na mwerevu. Mfalme alimpenda sana kwa kuwa mara kwa mara alikuwa akimpatia ushauri na kumfurahisha. Mwaka fulani mwezi wa 12, katika majira ya baridi theluji ilianguka sana, Dong Fangshuo alipomwona mfalme alikuwa hana raha, hivyo alikwenda kwenye bustani ili amchumie maua. Alipokuwa bustanini alimkuta mtumishi msichana mmoja, jina lake Yuan Xiao akilia kwa huzuni, na machozi yakimtiririka kwenye mashavu yake. Baada ya kumwuliza sababu, akatambua kwamba msichana huyo alikuwa na wazazi wawili wakongwe. Tangu msichana huyo achaguliwe kuwa mtumishi wa mfalme katika kasri, hakuwahi kuwaona. Kila ilipofika sikukuu ya mwaka mpya huwakumbuka sana. Dong Fangshuo baada ya kumfariji kidogo akamwahidi kumsaidia ili atoke kwenye kasri akaonane na wazazi wake.

Baada ya kumwacha mtumishi huyo wa kike Dong Fangshuo akaenda nyumbani kwa wazazi wake na kuwawekea mpango kwa akili yake. Dong Fangshuo aliondoka nyumbani kwa wazee akarudi mjini, huku akijifanya mpiga ramli barabarani. Kila aliyekuja kwake kupigiwa ramli alimwambia kwamba tarehe 15 Januari ni siku ya "kuunguzwa kwa moto mbinguni", na dawa ya kukwepa janga hili ni kuwa, "tarehe 13 mungu wa moto atajifanya msichana mwenye kuvaa mavazi mekundu akiwa na punda wa rangi nyekundu hafifu atakuja mjini Chang An kukagua sura ya ardhi, wakati huo wenyeji waende kaskazini ya mji wajipange barabarani ambapo msichana huyo atapitia, wamsihi wakilia na hivyo watu wote wataokoka." Watu waliambizana hayo na wakisubiri siku ya tarehe 13 iwadie. Siku ilipowadia, Dong Fangshuo alimwambia msichana mmoja aigize kama alivyomtaka, aliingia mjini taratibu akiwa juu ya punda wake. Wenyeji walipomwona wote walimvamia wakimsihi huku wakilia machozi. Msichana akawaambia, "Kutokana na ombi lenu, basi mkabidhi mfalme wenu kadi hii nyekundu aisome." Kisha akaondoka. Mfalme alifungua kadi akaona juu yake imeandikwa "Tarehe 15 moto utaanguka mbinguni, mji utaunguzwa." Baada ya kusoma hayo alitetemeka mwili mzima, asijue la kufanya. Kwa haraka akamwita Dong Fangshuo kumwomba ushauri wake. Kwa akili alimwambia mfalme, "Naomba mfalme wangu uwaambie raia wako waanze kutengeneza taa nyekundu toka leo na ifikapo siku ya tarehe 15 watundike barabarani, vichochoroni, milangoni, na kila mahali mjini; wawashe fataki na fashifashi na watu wa mjini na viungani watoke majumbani kuangalia; wewe mfalme na mkeo, mawaziri, masuria na watumishi wasichana, muende mjini pia mjumuike na raia kufurahia taa." Mfalme akatoa amri kama alivyoambiwa. Tarehe 15 usiku, taa ziling'ara kote mjini kama mchana, fataki na fashifashi zilikuwa zikitatarika angani. Kama walivyopangiwa wazazi walimwona binti yake Yuan Xiao, walipata nafasi ya kubadilishana nae mawazo kwa muda mrefu. Usiku wenye shamrashamra ulipita, mji mkuu wa Chang An ulisalimika, mfalme akafurahi sana. Akatoa amri, kwamba kila mwaka katika siku hiyo sherehe ifanyike kwa kutundika taa nyekundu na kuwasha fataki na fashifashi. Haya ndio masimulizi kuhusu chanzo cha Sikukuu ya Taa.

Baada ya sikukuu ya taa kuwa desturi ya Wachina siku hiyo haikuwahi kupuuzwa katika enzi zote za China. Siku hiyo taa hutengenezwa kwa aina na rangi mbalimbali, matengenezo ya taa ni sanaa maalumu za Kichina na baadhi ya sehemu hufanya maonyesho, taa za mayungiyungi, za kuelea majini, zenye vivuli vya wanyama vinavyozunguka zunguka, za majoka na barafu, zinavutia kwa ufundi mkubwa, watazamaji wanapostaajabu taa hizi huburudika na shamrashamra za michezo ya kuchezesha taa za majoka, ngoma ya mironjo, mashua ya nchi kavu, na kuonja vyakula vya sehemu maalumu.

Sikukuu ya Taa pia inamaanisha kumalizika kwa kipindi cha mwaka mpya wa Kichina.

Desturi za watu wa makabili madogomadogo ya China katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina

Sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina ni sikukuu ya pamoja kwa watu wa makabila 56 wa China. Mbali na kabila la wahan, watu makabila mengi madogomadogo pia wanasherehekea sikukuu hiyo kwa desturi zao maalum.

Kabila la wa-li (wengi wanaishi mkoani Hainan, kusini ya China): wakati wa siku ya mkesha wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, wa-li wa famili moja moja hukaa pamoja kunywa pombe na kula chakula, ambapo wanaimba nyimbo za kushangilia sikukuu. Tarehe 1 au 2 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, walii huenda pamoja kwa uwindaji, na wanyama waliokamata, nusu kumpa mlenga shabaha wa kwanza, nusu nyingine kugawanywa kwa watu wote, kila mmoja atapata mgao mmoja, na mjamzito anaweza kupata migao miwili.

Kabila la wa-yi (wengi wanaishi mkoani Sichuan, kusini magharibi ya China): Wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina wayii hucheza ngoma kwa pamoja, ngoma hiyo unaitwa "Axi aruka kwenye mwezi" ili kusherehekea sikukuu. Katika baadhi ya vijiji, tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, wanaume hufanya kazi za nyumbani na kuwaacha wanawake wapumzika siku hiyo, ili kuwapa pole kufanya kazi za nyumbani katika mwaka mmoja uliopita.

Kabila la wamiao (wengi wanaishi mikoani Hunan na Guizhou): wamiao huichukua sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina kuwa ni sikuuu ya "wakejia", kila familia huchinja nguruwe na kondoo, kuombea mvua na mavuno. Aidha wamiao huimba wimbo wa "Mwanzo wa siku ya kichipuka", wimbo huo unaonesha hisia za watu za kutarajia siku za kichipuka, na kutaka siku za kichipuka ziwe ndefu ili walime mashamba mazuri na kupata mavuno baadaye.

Kabila la waman (wengi wanaishi katika mikoa mitatu ya kaskazini mashariki pamoja na Beijing na mkoa wa Hebei): waman hupenda kusherehekea sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina mara mbili katika siku ya mkesha na siku ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo. Kabla ya sikukuu hiyo, waman hufanya mashindano ya kuruka kutoka kwenye farasi, na ngamia.

Kabila la watong (wengi wanaishi katika sehemu ya mkoa wa Guizhou, kusini magharibi ya China): watong hupenda kuvua samaki

asubuhi ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo na kuwaweka samaki hao hai kwenye meza ili kuonesha kuwa katika mwaka mpya familia itakuwa na baraka na chakula cha kutosha.

Kabila la wazhuan (wengi wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wazhuang la Guangxi, kusini magharibi ya China): wazhuang hupenda kupika chakula cha tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo usiku wa siku ya mkesha, kwa kuonesha kuwa mwaka unaofuata watakuwa na mavuno na baraka.

Kabila la waqiang (wengi wanaishi mkoani Sichuan, kusini magharibi ya China): wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, kila familia za waqiang huweka sadaka za ng'ombe na kondoo kwa kutambika kwa mababu. Aidha, katika usiku wa mkesha wa sikukuu, watu wote wa kila familia wakae pamoja kwa kuzunguka chungu cha pombe, mwenye umri mkubwa zaidi akinywa pombe kwanza kwa mrija wa mita moja halafu watu wa familia hiyo wanafyonza pombe kwa zamu toka kushoto hadi kulia.

Kabila la washui (wengi wanaishi mkoani wa Guizhou, kusini magharibi ya China): wakati wa sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, watoto wa kabila la washui wanaweza kuomba peremende kwa wazazi wa kila familia, nani atakaye pata peremende nyingi atachukuliwa kuwa ni mtoto mwenye heri na baraka zaidi, na siku za usoni atakuwa ni mwenye akili na afya nzuri.

Kabila la wabai (wengi wanaishi mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China): Asubuhi ya Tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo ya kichina, wabai wote wazee kwa watoto wa kila familia hunywa maji ya sukari yaliyotiwa mchele, hii inaonesha kuwa katika mwaka mpya wataishi maisha matamu.

Kabila la wakorea (wengi wanaishi katika mkoa wa Jilin, kaskazini mashariki ya China): Katika sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa kichina, watu wa kabila la wakorea wa kila familia wanabandika karatasi zilizoandikwa maneno ya kutakia heri na baraka za mwaka huu kwenye milango ya nyumba, kupika vyakula vingi vya aina mbalimbali. Na asubuhi mapema ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, watu huamka na kuvaa nguo maridadi ya sikukuu na kutoa heshima kwa wazee na wazazi na kuwatakia heri na baraka za mwaka mpya.

Kabila la wamongolia (wengi wanaishi katika mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani ya kaskazini magharibi ya China): Asubuhi ya tarehe 1 mwezi wa kwanza kwa kalenda ya kilimo, vijana wa kiume na kike wanaovaa nguo maridadi za aina mbalimbali hupanda farasi kwenda nyumbani kwa wazazi wa kila familia kutoa heshima na kuwatakia heri na baraka za mwaka mpya. Aidha, kabila la wamongolia hufanya tamasha kubwa la kuimba nyimbo na kucheza ngoma, ambapo watu wote wanavaa vibandiko kwenye nyuso zao, ili kuonesha kuagana na mwaka uliopita na kukaribisha mwaka mpya.

Kabila la wahani (wengi wanaishi mkoani Yunnan, kusini magharibi ya China): vijana wa kiume na kike wa kabila la wahani hukusanyika pamoja wakati wa mwaka mpya wa jadi wa kichina, wakinywa pombe, kuimba nyimbo, kucheza dansi na kuwachagua wachumba.

Kabila la Wanaxi (mkoani Yunnan, kusini magharibi mwa China): Katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina, watoto wa kiume wanaotimiza miaka 13 wanafanyiwa "sherehe ya kuvaa suruali" na watoto wa kike wanafanyiwa "sherehe ya kuvaa sketi", ikimaanisha kuwa watoto hao wameingia katika utu uzima.

Kabila la Wapumi (mikoani Yunnan na Sichuan, kusini magharibi mwa China):

Asubuhi katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina watu wa kabila la Wapumi wanapiga mizinga na mbiu kuusherehekea mwaka mpya.

Kabila la Wabuyi (mkoani Guizhou, kusini magharibi mwa China):

Katika siku za mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila hilo huvaa mavazi ya sikukuu kusalimiana au kwenda kufanya utalii, kuimba na kucheza ngoma vya kutosha, kisha wanarudi nyumbani.

Kabila la Waoroqen (mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China):

Asubuhi mapema katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila hilo huwamiminia wazee wa familia yao glasi nzima ya mvinyo wakionesha heshima, kisha vijana hao wanatakiana heri kwa kunywa mvinyo. Baada ya kifungua kinywa vijana hukusanyika pamoja kufanya mashindano ya mbio za farasi na kulenga shabaha kwa mishale.

Kabila la Wadaur (mkoani Heilongjiang, kaskazini mashariki mwa China):

Asubuhi mapema katika siku ya kwanza ya mwaka mpya wa Kichina vijana wa kabila la Wadaur huwa wanapaka masizi na kuwapakia wengine usoni wakiwemo wasichana. Inasemekana kuwa kufanya hivyo kuna maana ya kuwatakia furaha na mavuno mazuri ya kilimo.

Siku ya 8 Desemba

Tarehe 8 Desemba katika kalenda ya Kichina ni siku ya jadi ya kabila la Wahan ambayo pia inaashiria sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina kukaribia.

Kutokanna na maandishi ya kale, siku ya 8 Desemba katika kalenda ya Kichina ni siku ya kufanya tambiko katika China ya kale. China ni nchi inayotilia maanani sana kilimo. Kila mwaka mavuno mazuri yalipopatikana watu wa kale walikuwa wanafanya tambiko ili kumshukuru mungu. Baada ya tambiko watu hukusanyika kufanya sherehe za burudani, kupika uji wa mseto na kula pamoja. Katika karne ya 5 serikali ya enzi zile iliweka siku hiyo yaani 8 Desemba kuwa ni sikukuu.

Baada ya dini ya Buddha kuingia nchini China, maana ya siku hiyo ya 8 Desemba ilikuwa imeongezeka. Inasemekana kwamba baada ya Sakyamuni kuwa Buddha alikuwa na maisha magumu, na alikonda vibaya. Katika siku hiyo alimkuta mchungaji msichana ambaye alimpa bakuli moja la uji wa mseto kutokana na kuona jinsi alivyokonda. Kwa hiyo waumini wa dini wa Buddha pia wanapika uji wa mseto katika siku hiyo.

Watu wa China wana desturi ya kunywa uji wa mseto kuanzia Enzi ya Song yaani miaka elfu moja iliyopita. Katika siku hiyo ya 8 Desema kila familia na hata maofisa wa serikali walikuwa wanakunywa uji wenye mchanganyiko wa mchele na kunde.

Aina za uji wa mseto ni nyingi kutokana michele na kunde tofauti zilizotiwa ndani ya uji, lakini kwa kawaida huwa ni mchele, muwele, ngano na mahindi, mtama, choroko, maharage na kunde nyekundu.

Vitu vilivyokuwa vinatiwa ndani ya uji pia kulikuwa na matunda yaliyokaushwa, na mbegu za matunda kama karanga, njugumawe, alizeti, zabibu, tende, n.k.

Baada ya vitu vyote kuwa tayari, uji hupikwa kwa moto mdogo na kwa muda mrefu. Katika majira ya baridi jamaa wanajikusanya pamoja kando ya meza na kunywa uji kama huo.

Wenyeji wa Beijing wanaichukulia siku hiyo kama ni ishara ya kukaribia kwa sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina. Licha ya kunywa uji wa mseto, katika siku hiyo watu hutia saumu ndani ya siki ili watumie katika mkesha mwaka mpya wakati wanapokula Jiaozi , chakula kama sambusa ndogo kilichochemshwa.

Masimulizi kuhusu mkesha wa mwaka mpya

Usiku wa siku ya mwisho ya Desemba katika kalenda ya Kichina ni mkesha sikukuu ya mwaka mpya wa Kichina.

Katika usiku huo wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya, mila na desturi za Wachina ni nyingi. Moja ni kufagia nyumba. Kabla ya kufikia siku ya mwisho ya mwaka watu hufagia nyumba kwa maana ya kuondoa uchafu na kusherehekea mwaka mpya katika hali ya kila kitu kuwa safi.

Baada ya kusafisha, wanapamba nyumba kwa maandishi yenye maneno ya kuomba baraka na picha, na kutundika taa nyekundu.

Katika mkesha wa mwaka mpya, jamaa hula pamoja, hata fulani akiwa mbali kwa kazi lakini katika siku hiyo hurudi nyumbani kujumuika na jamaa zake na kula nao pamoja.

Chakula cha usiku wa kuamkia sikukuu ya mwaka mpya katika sehemu ya kusini na sehemu ya kaskazini ni tofauti. Watu wa sehemu ya kusini hupika vitoweo vingi zaidi na kumi na watu wa sehemu ya kaskazini wana mila ya kula Jiaozi kwa kuchovya kwenye siki iliyotiwa saumu.

Katika usiku huo watu wazima huwachukua watoto na kwenda nao kwa jamaa na kuwapelekea zawadi, na watoto katika usiku huo wanawasibiliza wazee wosia wao. Katika usiku huo watoto hupewa fedha ambazo zinaitwa "fedha za kuaga mwaka". Si wazee si watoto, katika usiku huo hawalali, baada ya chakula, wanaongea huku wana wanakunywa chai na kula vyakula vya udohodoho na kuangalia michezo ya televisheni mpaka alfajiri.

Katika usiku huo watoto huwa na furaha tele, wanapitisha usiku huo wakiwa pamoja na wazee na kuwasha fataki. Mshairi mkubwa wa China ya kale aliwahi kueleza watoto walivyokuwa katika usiku huo "Watoto wavumilia usingizi na kuwa na furaha hadi alfajiri".


1 2 3 4