6: Makabila na Dini

Hali ya Dini Nchini China

China ni nchi yenye dini mbalimbali. Waumini wa dini wa China niwa dini za kibudha, kidao, kiislamu, na kikristo.

Kutokana na takwimu zisizokamilika, hivi sasa China ina waumini zaidi ya milioni 100 wa dini za aina mbalimbali, makanisa, misikiti na mahekalu zaidi ya elfu 85, wafanyakazi wa shughuli za kidini laki tatu, vikundi zaidi ya 3000 na vyuo 74 vya kidini.

Nchini China, kuna Shirikisho la Dini ya kibudha la China, Shirikisho la Dini ya Kidao la China, Shirikisho la Dini ya Kiislamu la China, Shirikisho la Dini ya Uzalendo la Kikatoliki la China, Jumuiya ya Maaskofu wa Katoliki ya China, Kamati ya Harakati za Uzalendo ya Dini ya Kikristo ya China na Shirikisho la Ukristo ya China. Mashirika mbalimbali ya kidini yanachagua viongozi na kuunda miundo ya utawala kutokana katiba zao yenyewe; yanashughulikia mambo yao ya kidini kwa kujiendesha, kuanzisha vyuo vya kidini kutokana na mahitaji yao, kuchapisha vitabu vya kidini na majarida ya kidini na kuanzisha shughuli za kuhudumia jamii.

Dini Nchini China

Dini ya kibudha

Dini ya kibudha ilienea nchini China kuanzia karne ya kwanza baada ya kuzaliwa kwa Kristo, na ilianza kuenea kote nchini China baada ya karne ya nne, na imekuwa dini yenye athari kubwa zaidi nchini China. Dini ya kibudha ya China iliundwa na mifumo mitatu ya lugha ya Kihan, lugha ya Kitibet na lugha ya Kipali, kwa jumla kuna watawa wa kiume laki mbili. Hivi sasa China ina mahekalu zaidi ya 13000 ya dini ya kibudha yaliyo wazi kwa waumini, vyuo 33 vya dini ya kibudha na vitabu au majarida 50 ya kibudha.

Dini ya kibudha la Kitibet ina waumini wengi katika mkoa unaojiendesha wa Tibet , mkoa unaojiendesha wa Mongolia ya ndani na mkoa wa Qinghai. Makabila ya watibet, wamongolia, wa-uygur, wamenba, waluoba na wa-tu ni waumini wa dini ya kibudha ya kitibet, waumini Qke wamefikia zaidi ya milioni 7. Dini ya kibudha ya Kipali huenea kwenye wilaya inayojiendesha ya kabila la wadai ya Xishuanbanna, wilaya inayojiendesha ya kabila la wadai na wajinbo ya sehemu ya Dehong na sehemu ya Simao ya mkoa wa Yunnan, kusini magharibi mwa China. Idadi kubwa ya watu wa makabila ya wadai, wabulang, waachang na wa-wa ni waumini wa dini hiyo, waumini wake wamefikia zaidi ya milioni moja. Waumini wa dini ya kibudha ya kihan wanatapakaa nchini kote.

hekalu maarufu la dini ya kibudha mkoani Zhejiang--Hekalu la Lingshi la Ningpo

Dini ya Kidao

Dini ya Kidao ni dini ya kienyeji nchini China, ilianza kuwepo katika karne ya pili, imekuwa na historia ya zaidi ya miaka 1800. Dini hiyo inarithi dini ya kale ya kuabudu maumbile na wababu, ilikuwa na madhehebu mengi. Madhehebu hayo yaliendelea taratibu na kuundwa kuwa madhehebu mawili makuu ya Dao ya Quanzhen na Zhengyi, waumini wengi wa dini hiyo ni wa kabila la wahan. Kutokana na kuwa Dini ya Kidao haina matambiko na utaratibu wa ibada, hivyo ni vigumu kufahamu idadi kamili ya waumini wake. Hivi sasa China ina mahekalu 1500 ya dini ya Kidao, na watawa wa kiume na kike zaidi ya elfu 25.

Dini ya Kiislam

Dini ya kiislamu ilienea nchini China katika karne ya 7. Wakazi wengi wa makabila ya wahui, wauigur, watatar, wakerkez, wakazakh, wauzbek, wadongxiang, wasala, na wabaoan wenye idadi ya watu zaidi ya milioni 18 ni waumiuni wa dini ya Kiislam. Waumini wengi wa dini ya kiislamu wa China huishi katika mkoa unaojiendesha wa kabila la wauigur wa Xingjiang, mkoa unaojiendesha wa kabila la wahui wa Ningxia, na mikoa ya Gansu, Qinghai na Yunnan, lakini pia kuna waumini wa dini ya kiislamu katika sehemu nyingine nchini China. Hivi sasa China ina misikiti zaidi ya elfu 30, na maimamu zaidi ya elfu 40.

Madhehebu ya Kikatoliki

Madhehebu ya kikatoliki yalienea nchini China kwa mara ya kwanza katika karne ya 7, hasa baada ya vita ya kasumba mwaka 1840. Hivi sasa Jumuiya ya kikatoliki ya China ina parokia 100, waumini wamefikia milioni tano hivi, makanisa 5000, na vyuo 12 vya kidini. Katika miaka 20 iliyopita, Jumuiya ya kikatoliki ya China imewaandaa padre vijana zaidi ya 1500, kati yao mapadre vijana zaidi ya 100 wamepelekwa kupiga msasa katika nchi za nje. Zaidi ya hayo, Jumuiya ya kikatoliki ya China pia imewaandikisha watawa vijana wa kike 3000. Makanisa ya kikatoliki nchini China kila mwaka yanawabatiza watu elfu 50, kwa ujumla Biblia zaidi ya milioni tatu zimechapishwa.

kanisa la Ukatoliki lililoko mtaa wa Wangfujin, Beijing

Dini ya Kikristo Dini ya Kikristo ilifika nchini China mwanzoni mwa karne 19, na kuenea zaidi baada ya vita ya kasumba mwaka 1840. Mwaka 1950, ya Kikristo ilianzisha harakati za kuondoa athari ya ubeberu, na kuandaa moyo wa uzalendo, kufanya juhudi kwa ajili ya kutimiza lengo la wakristo wa China wajiendeshe, kujitegemea na kueneza dini yao. Hivi sasa China ina wakristo milioni 10, mapadre zaidi ya elfu 18, makanisa elfu 12, na sehemu nyingine elfu 25 za kufanyia shughuli za kidini.


1 2 3 4 5 6