10: Kisiwa cha Taiwan

Miji mikubwa

Mji wa Taibei

Mji wa Taibei uko katika sehemu ya kaskazini ya Kisiwa cha Taiwan, eneo la mji huo mzima ni kilomita za mraba 272, ambao ni mji wa kwanza kwa ukubwa kisiwani humo. Idadi ya watu wake ni milioni 2.7, hii ni 12.5 % ya idadi ya jumla ya watu wa kisiwa kizima cha Taiwan.

Taibei ni kituo cha viwanda na biashara cha Taiwan, makampuni na mashirika makubwa, mabenki na maduka makubwa ya Taiwan mengi yameweka makao makuu yao huko Taibei. Mji wa Taibei ukiwemo pamoja na wilaya za Taibei, Tiaoyuan na Jilong, ambao ni sehemu kubwa zaidi ya uzalishaji wa viwanda na shughuli za biashara kisiwani Taiwan.

Taibei pia ni kituo cha utamaduni na elimu cha Taiwan. Vyuo vikuu 24 kama vile Chuo kikuu maarufu cha Taiwan, Chuo kikuu cha siasa cha Taiwan na Chuo kikuu cha ualimu cha Taiwan viko huko. Aidha, vituo vya habari, uchapishaji, matangazo na televisheni na maktaba kubwa zaidi na Jumba kubwa zaidi la makumbusho pia yako huko.

Mjini Taibei hali ya mawasiliano ni nzuri, mji huo ni moja kati ya vituo vya reli na barabara vya Taiwan. Bandari la Jilonglong na Bandari la maji baridi ni milango ya Taibei ya kuelekea baharini. Uwanja wa ndege wa Songshan wa Taibei ni uwanja mkubwa wa pili wa ndege wa kimataifa wa Taiwan.

Mji wa Gaoxiong

Mji wa Gaoxiong una eneo la kilomita za mraba 150 hivi, idadi ya watu wake ni zaidi ya milioni 1.4 kwa hivi sasa. Huu ni mji ulioendelea mapema zaidi, wenye historia ndefu zaidi na uliendelea haraka katika sekta za viwanda na biashara.

Mji wa Gaoxiong ni kituo kikubwa cha viwanda cha Taiwan, katika mji huo kuna viwanda vikubwa zaidi vya Taiwan kama vile vya kusafisha mafuta, chuma na chuma cha pua, na kutengeneza meli, pia kuna viwanda vya elektroniki, viwanda vya kutengeneza mashine na mitambo, viwanda vya saruji na mbolea za chumvichumvi, viwanda vya kuyeyusha aluminium, na vya kutengeneza sukari, shughuli hizo ziliendelea sana huko. Gaoxiong pia ni kituo cha uzalishaji wa mazao ya samaki cha Taiwan, na shughuli zake za kuvua samaki kwenye bahari ya mbali zinaongoza zile za mkoa mzima.

Mjini Gaoxiong mawasiliano ya baharini, barabarani na angani yote yaliendelea sana. Huko kuna Bandari nzuri ya Gaoxiong ambayo inaweza kuegesha kwa wakati mmoja meli kubwa 38 za uzito wa tani elfu 10. Bidhaa zinazoingia na kutoka bandari hiyo ni nyingi na kuchukua nafasi ya 4 duniani kuifuata Hong Kong, Singapore, na Rotterdam, Uholanzi. Uwanja wa ndege wa Gaoxiong una safari malaum na zisizo malaum za kimataifa na za kisiwani humo. Kwenda Gaoxiong kutoka Taibei, kupanda ndege kunachukua muda wa dakika 40 tu, kwa gari moshi au magari kunachukua muda wa saa 4.

Mji wa Gaoxiong pia ni mji mzuri sana, siku zote ni za joto, hakuna siku za baridi, majira manne ya mwaka yanaonesha mandhari ya kanda ya tropiki.

Miji mitano inayotawaliwa moja kwa moja na mkoa

Mji wa Taizhong

Mji huo uko katika sehemu ya magharibi ya Kisiwa cha Taiwan, ambao ni mji wa tatu kwa ukubwa wake kisiwani humo. Hivi sasa mji huo umekuwa kituo cha utamaduni na elimu, uchumi na mawasiliano katika sehemu ya kati ya Taiwan. Vyuo vikuu vya mji huo ni vingi kwa vikiufuatia mji wa Taibei. Mji huo pia ni kituo cha utamaduni wa dini ya budha cha Taiwan, kila mwaka mkutano wa shughuli za dini ya budha wa Taiwan unafanyika katika Hekalu la Baojue mjini humo. Mji wa Taizhong siku zote unadumisha sura nadhifu na usafi, ambao unasifiwa kuwa ni mji msafi zaidi kuliko mingine huko Taiwan.

Mji wa Tainan

Mji huo uko kwenye kando ya bahari ya kusini magharibi ya kisiwa cha Taiwan, ambao ni mji wa 4 kwa ukubwa wake, pia ni mji wa kale zaidi kisiwani Taiwan. Kabla ya mji wa Taibei kufanywa kuwa mji mkuu wa mkoa wa Taiwan, mji wa Tainan ulikuwa kituo cha kisiasa, kiuchumi na utamaduni cha Taiwan. Mjini humo kuna vivutio vingi na mabaki mengi ya kale. Na mji wa Tainan pia ni mji uliojaa harufu nzito ya kidini, kote mjini kuna mahekalu na makanisa zaidi ya 200, na waumini wa dini ya budha na dini ya dao ni wengi zaidi, pia wapo waumini wengi wa dini ya kristo.

Mji wa Jilong

Mji huo uko kaskazini ya Kisiwa cha Taiwan, ambao unakabiliana na Bahari ya mashariki, huu ni mji wa bandari unaozungukwa na milima. Mji huo ni moja kati ya sehemu zilizoendelea mapema zaidi kisiwani humo, ambapo hali ya mawasiliano iliendelea sana, na viwanda vya kuunda meli, viwanda vya kemikali, makaa ya mawe na viwanda vya kutengeneza mazao ya majini pia vilisitawi sana. Sehemu hiyo pia ni bandari moja kubwa ya uvuvi, utoaji wa samaki wa sehemu hiyo unachukua 20 % ya ule wa jumla wa Taiwan. Na katika mji huo, mvua inanyesha kwa siku zaidi ya 200 kwa mwaka, hiyo, mji huo huitwa kuwa "Bandari ya mvua".

Mji wa Xinzhu

Mji huo uko wilayani Xinzhu, ambao ni mji muhimu wa sayansi na utamaduni kwenye pwani ya magharibi ya Taiwan. Vyuo vikuu maarufu vya Taiwan kama vile Chuo kikuu cha Qinghua na Chuo kikuu cha mawasiliano na Sehemu ya viwanda vya kisayansi ya Xinzhu vyote viko katika mji huo.

Mji wa Jiayi

Mji huo uko wilayani Jiayi. Bwawa la Zengwen ambalo ni kubwa zaidi kuliko mengine ya Taiwan liko jijini humo.


1 2 3 4 5 6 7 8