10: Kisiwa cha Taiwan

Sera ya serikali ya China ya utatuzi wa suala la Taiwan

Sera ya kimsingi ya serikali ya China kuhusu utatuzi wa suala la Taiwan ni: "muungano wa amani, nchi moja mifumo miwili".

Mapema katika miaka ya 50 ya karne iliyopita, serikali ya China iliwahi kuzingatia kutatua suala la Taiwan kwa njia ya amani. Tarehe 1 Januari, 1979, Halamashauri ya kudumu ya Bunge la umma la Jamhuri ya watu wa China ilitoa "Taarifa kwa ndugu wa Taiwan", taarifa hiyo ilizitaka pande mbili zikomeshe hali ya kukabiliana kijeshi na kufanya mazungumzo. Taarifa hiyo ilisema kuwa wakati wa kutimiza muungano wa taifa, lazima "kuheshimu hali ilivyo ya Taiwan, na kuchukua sera na njia mwafaka kwa kufuata hali halisi".

Tarehe 30 Septemba, 1981, Spika wa Bunge la umma la China Ye Jianying alitoa tamko akifafanua zaidi sera ya China ya kutatua suala la Taiwan. Alisema kuwa, "baada ya kutimiza muungano wa taifa, Taiwan itaweza kuwa mkoa wa utawala maalum ambao utakuwa na madaraka ya juu ya kujiendesha".

Mwaka wa pili baada ya hapo, kiongozi wa China Deng Xiaoping alitoa tamko juu ya maneno yaliyosemwa na Ye Jianying akidhihirisha kuwa, hoja hii kwa kweli ni kuhusu "nchi moja mifumo miwili", chini ya msingi wa muungano wa taifa, mfumo wa ujamaa unatekelezwa kwenye eneo kubwa la nchi, na Taiwan itekeleze mfumo wa kibepari.

Tarehe 12 Oktoba,1992, katibu mkuu wa wakati huo wa kamati kuu ya Chama cha kikomunisti cha China Jiang Zemin alidhihirisha kuwa, "Sisi tunafuata kithabiti sera ya 'Muungano wa amani, nchi moja mifumo miwili', na kufanya juhudi za kuhimiza muungano wa taifa".

Yaliyomo ya sera ya "Muungano wa amani, nchi moja mifumo miwili"

Yaliyomo ya kimsingi ya Sera ya serikali ya China ya utatuzi wa suala la Taiwan ya "Muungano wa amani, nchi moja mifumo miwili" ni kama yafuatayo:

Kuwepo kwa China moja: Kuna China moja duniani, Taiwan ni sehemu moja siyotengeka ya China, serikali kuu iko Beijing. Hili ni sharti la kwanza la kutatua kiamani suala la Taiwan.

Kuwepo kwa mifumo miwili: Kwenye msingi wa kuwepo kwa China moja, mfumo wa ujamaa wa China bara na mfumo wa kibepari wa Taiwan itakuwepo kwa pamoja kwa muda mrefu na kuendelea kwa pamoja.

Kujiendesha kwenye kiwango cha juu: Baada ya kutimiza muungano wa taifa, Taiwan itakuwa mkoa wa utawala maalum. Mkoa huo utatofautiana na mikoa mingine ya kawaida ya China, utakuwa na madakara ya juu ya kujiendesha.

Kufanya mazungumzo ya amani: Kutokana na hali ilivyo ya sasa ya pande mbili za China bara na Taiwan, serikali ya China inatetea kuwa kabla ya kutimiza muungano wa taifana, pande hizo mbili zifuate kanuni za kuheshimiana, kusaidiana na kunufaishana, kufanya juhudi za kusukuma mbele ushirikaino wa kiuchumi na mawasiliano mbalimbali kati ya pande hizo mbili, kufanya mawasiliano ya moja kwa moja katika sekta ya posta, biashara, usafiri na maingiliano kati ya pande hizo mbili, ili kuweka mazingira ya kutimiza muungano wa amani wa taifa.


1 2 3 4 5 6 7 8