20: Makumbusho kwenye Mtandao

Picha za Kale

Picha ya "Mandhari Nzuri ya Taoyuan kama ya Peponi" na Mchoraji Wake Chou Ying

Chou Ying (1493-1560), alikuwa mwenyeji wa sehemu ya Taicang mkoani Jiangsu. Awali alikuwa mpaka vanishi kwenye samani, na baadaye alijifunza uchoraji picha kwa mwalimu wake Zhou Chen.

Picha hiyo ilichorwa mandhari iliyojitenga na dunia yenye ghasia na kuonesha sehemu ya maisha yenye mandhari ya milima, mito, miti na madaraja. Watu katika picha hiyo ni muhimu.

Picha ya "Kurudi Nyumbani kwa Kupanda Punda"

Picha hiyo ilichorwa na Tang Bohu (1470-1523) wa Enzi ya Tang. Alikuwa mwenyeji wa mji wa Suzhou mkoani Jiangsu. Alikuwa hodari wa kuandika mashairi na kuchora picha. Alipokuwa mzee alianza kuamini dini ya Buddha.

Katika picha hiyo ilichorwa njia nyembamba vichakani, nyumba hapa na pale, mito iliyotiririka mlimani wenye miti mingi, na mtu mmoja aliyepanda punda akielekea nyumbani.


1 2 3 4