-
Kipi ni chakula maarufu kwenye mkahawa huu?
Kwa kawaida, watu wakienda mkahawa wa kichina kula chakula huwa wanaweza kumwuliza mhudumu wa mkahawa: Kipi ni chakula maarufu kwenye mkahawa huu? Kwani kuna aina mbalimbali za mapishi ya vyakula vya kichina, hata vyakula hivyo vina ladha tofauti, na mapishi hayo tofauti huhusiana na umaalum wa sehemu mbalimbali tofauti . Kwa mfano, vyakula vilivyopikwa kwenye mikahawa ya mkoani Sichuan huwa vina ladha ya pilipili hoho, na vile vilivyopikwa mjini Shanghai huwa vina ladha ya sukari zaidi. Hivyo unatakiwa kuuliza: Ni men you shen me te se cai?Kipi ni chakula maarufu kwenye mkahawa huu?
Ni men, nyinyi,
you, kuwa na,
shen me, kipi,
te se, umaalum,
cai,chakula.
-
Unataka kupata vijiko?
labda watu wengi wanajua, vijiti vya kulia ni kitu maalum kinachotumiwa na wachina kula chakula. Wageni wengi wanaokuja China hawafahamu kutumia vijiti vya kulia badala ya vijiko, hivyo wahudumu wanaweza kuwauliza Ni xu yao dao cha ma?
xu yao, hitaji,
dao, kisu, cha, vijiko,
ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Tafadhali niambie, unataka chai nyekundu?
Chai ya China inajulikana sana, kama ukimwalika rafiki yako mchina kwenda kwenye mkahawa wa chakula cha Kichina, ukitaka kumwuliza kama anataka kunywa chai nyekundu, utamwuliza : Qing wen ni yao hong cha ma?
Qing, tafadhali,
wen, kuuliza,
Qing wen, tafadhali niambie,
ni, wewe,
yao, kutaka,
hong cha, chai nyekundu,
ma, kisaidizi cha neno kwa kuuliza.
-
Tugawanye malipo kila mmoja atoe sehemu moja.
Siku hizi vijana wa China wanapokula pamoja kwenye mkahawa, wengi wao wanafuata utaratibu wa AA, yaani malipo ya chakula yatalipwa kwa kila mtu kuchangia sehemu moja, ambapo wanaweza kusema: wo men AA zhi ba.
wo men, sisi,
AA zhi, utaratibu wa AA,
ba, kisaidizi cha neno.