-
Nafurahi kufahamiana na watu wa familia yako.
Ukienda nyumbani kwa rafiki yako wa kichina, unaweza kusema"wo hen gao xing ren shi ni de jia ren." wo, mimi, hen, sana, gao xing, kufurahi, ren shi, kufahamiana, ni de, yako, jia ren, familia.
-
Hiki ni kitoweo nilichopika vizuri.
Wakati ukiwa mgeni wa nyumbani kwa wachina, wachina hupenda kukupikia chakula kitamu, na wanataka wewe uonje na kukwambia: :zhe shi wo de na shou cai. Hiki ni kitoweo nilichopika vizuri. zhe, hiki, shi, ni, wo de, changu, na shou, kufanya vizuri, cai, chakula.
-
Ule zaidi.
Wakati wa kula chakula nyumbani kwa wachina, wachina huweza kukutaka ule chakula kingi zaidi, husema ni duo chi dian er. Ule zaidi. ni, wewe, duo, nyingi,chi, kula, dian er, kidogo.
-
Siku zijazo mnakaribishwa nyumbani kwangu.
Ukiondoka nyumbani kwa rafiki yako wa kichina, unaweza kusema: Xia ci qing ni men dao wo jia zuo ke. Xia ci, mara ijayo, qing,tafadhali, ni men, ninyi, dao,kuja, wo jia, nyumbani kwangu, zuo ke,kuwa mgeni.