somo 16 katika mkusanyiko wa familia

 ongea na CRI
 

Kwa mujibu wa kalenda ya kilimo ya China, tarehe 1 ya mwezi wa kwanza ni sikukuu ya mwaka mpya wa jadi wa China. Hii ni sikukuu kubwa zaidi kwa wachina. Kwa kufuata mila na desturi za wachina, kabla ya sikukuu hiyo, watu husafirisha nyumba na kupamba nyumba ili kukaribisha mwaka mpya, ambapo watu hupenda kubandika “chun lian” yaani karatasi mbili nyekundu zilizoandikwa maneno ya kutakia heri na banaka, au kubandika karatasi nyekundu yenye neno “福”(fu) juu ya mlango, wengi hupenda kubandika neno “福” juu chini, kumaanisha baraka imefika. Kadhalika kubandika picha ya mungu anayeshughulikia mambo ya fedha kwa matarajio ya kuongeza mapato.