somo 17 katika dhifa

 ongea na CRI
 

Kuwa na unyenyekevu ni tabia nzuri ya jadi ya wachina. Wachina wanaona kuwa kama mtu anajivunia sana huweza kupata madhara; na mtu anayependa kusikiliza maoni na ushauri wa wengine ni mtu mwenye adabu. Hivyo wachina wengi hawapendi kujivunia baada ya kusifiwa na mtu, ambapo wanapenda kusema: "过奖了"(guo jiang le), au "我做得还很不够"(wo zuo de hai hen bu gou), maana yake ni bado sijafanya vizuri sana, ninatakiwa kufanya bidii zaidi.