somo 2 kushukuru na kuomba radhi

 ongea na CRI
 
  • angalia
  • kujifunza
  • mazoezi
  • 正常播放   谢谢!谢谢你!Xièxie! Xièxie nǐ!

    Asante.
    A. Kama unataka kumshukuru mtu, unaweza kusema "xiè xiè". "xiè xiè" inamaanisha asante. Ama unaweza kusema "xiè xiè nĭ". "nĭ": wewe.
  • 正常播放   非常感谢!Fēicháng gǎnxiè!

    Asante sana!
    Kama unataka kumshukuru sana, unaweza kusema "fēi cháng găn xiè", asante sana. Neno "fēi cháng" ni kisaidizi cha neno, maana yake ni sana."găn xiè" pia inamaanisha "asante".
  • 正常播放   不用谢!Bú yòng xiè!

    Bila asante!
    Kama mtu fulani anakushukuru akisema "xiè xiè", unajua kumjibu nini? Kwa Kiswahili tunasema bila asante, Kichina tunasema, "bú yòng xiè", maana yake ni hiyo hiyo: bila asante."bú yòng" inamaanisha hakuna haja, "xiè" inamaanisha asante.
  • 正常播放  慢速播放  A:非常感谢!
    Fēicháng gǎnxiè!
    Asante sana!
  • 正常播放  慢速播放  B:不用谢!
    Bú yòngxiè!
    Bila asante!