-
Asante.
A. Kama unataka kumshukuru mtu, unaweza kusema "xiè xiè". "xiè xiè" inamaanisha asante. Ama unaweza kusema "xiè xiè nĭ". "nĭ": wewe.
-
Asante sana!
Kama unataka kumshukuru sana, unaweza kusema "fēi cháng găn xiè", asante sana. Neno "fēi cháng" ni kisaidizi cha neno, maana yake ni sana."găn xiè" pia inamaanisha "asante".
-
Bila asante!
Kama mtu fulani anakushukuru akisema "xiè xiè", unajua kumjibu nini? Kwa Kiswahili tunasema bila asante, Kichina tunasema, "bú yòng xiè", maana yake ni hiyo hiyo: bila asante."bú yòng" inamaanisha hakuna haja, "xiè" inamaanisha asante.
-
Samahani.
Namna ya kuomba radhi kwa Kichina . Samahani kwa Kichina ni "duì bù qĭ ".
-
Si kitu. Usijali.
Na kama mtu mwingine alikuambia "duì bù qĭ ", utaamjibu "méi guān xì", si kitu, usijali."méi": si.
-
Si kitu. Usijali.
Mbali na "méi guān xì" , pia unaweza kusema, "méi shì er",maana yake ya Kichina ni hiyo hiyo, si kitu, usijali."méi": hakuna, "shì er" mambo.