somo 20 katika soko la bidhaa zilizotumika

 ongea na CRI
 

  • Hii ni ya chapa gani? Ukienda sokoni kununua pikipiki ambayo labda siyo mpya, kwanza ni lazima uulize pikipiki hiyo ni ya chapa gani, unaweza kusema: zhe shi shen me pai zi de? Hii ni ya chapa gani?
    Zhe, hii, Shi, ni, shen me, gani, pai zi,chapa, de, kisaidizi cha neno.

  • Hii ni ya chapa maarufu ya China
    Hivi sasa bidhaa nyingi zinachapishwa maneno ya "made in China" duniani. Kuna chapa nyingi maarufu imekuwa na sifa yao duniani, kama "Haier". Chapa maarufu kwa Kichina ni: zhong guo ming pai. zhong guo,China, ming pai, chapa maarufu.

  • Hapa kuna dosari.
    Ukinunua pikipiki isiyo mpya, hata kama ni ya chapa maarufu, pia inaweza kuwa na dosari, kwanza ungeichunguza kwa makini. Halafu unaweza kumwambia muuzaji: zhe er you dian er mao bing,hapa kuna dosari. Zhe er, hapa, mao bing, dosari, you dian er mao bing,kuna dosari ndogo.

  • Chini ya Yuan 100
    Zui duo, chini ya, yi bai yuan, mia moja, zui duo yi bai yuan, zisizozidi Yuan 100.