Unaweza kupatana bei kwenye baadhi ya maduka binafsi ya China. Na baadhi ya watu wanapenda kupatana bei. Kuna njia mbalimbali za kupatana bei. 1. Usimwambie muuzaji dukani vitu unavyovihitaji kwelikweli. Ukienda kununua vitu, unatembelea kwanza, na unauliza na kupatana bei katika maduka tofauti, halafu ukajua duka lipi linauza kwa bei nafuu. 2. Ujitahidi kudhihirisha dosari za bidhaa. Hakuna bidhaa zisizo na upungufu wake. Muuzaji hukuambia bidhaa nzuri tu, wakati huo ni lazima uthibitishe dosari zake. Yaliyosema hapa juu ni katika hali ulipokwenda maduka binafsi ya China, ukienda maduka makubwa ya China, bei za bidhaa huamuliwa bila kupunguzwa.