somo 22 katika duka la nguo

 ongea na CRI
 

  • Nataka kununua gauni moja la Qipao.
    Gauni la kichina liitwalo Qipao ni nguo ya jadi ya China, na wanawake wa China wanapenda kuivaa. Kama ukitaka kumnunulia mama yako, ukienda dukani utamwambia muuza duka: wo xiang mai yi jian qi pao.
    wo: mimi. xiang: taka. mai: nunua. yi jian Qipao: gauni moja la Qipao.

  • Hiki ni kitambaa cha aina gani?
    Zhe: hiki, shi: ni, shen me: nini, liao zi: kitambaa, de: kisaidizi cha neno.

  • kati ya nguo ya rangi ya buluu na ya rangi ya manjano, ipi inapendeza zaidi?
    ukichagua rangi ya nguo, unaweza kumwomba rafiki yako atoe ushauri wake, au kumwuliza mhudumu. Unaweza kusema: lan se de hao hai shi huang se de hao? lan se de: rangi ya buluu, hai shi: au, huang se de: rangi ya manjano, hao: nzuri.

  • Naweza kujaribu kuvaa nguo hii?
    kama wewe umenunua nguo, na una wasiwasi kuwa labda nguo hiyo haitakufaa, unaweza kuomba kujaribu kabla ya kununua, unaweza kusema: neng shi shi ma? Naweza kujaribu kuvaa nguo hii?
    Neng: weza. Shi shi: jaribu. Ma: neno la kisaidizi kwa kuuliza.

  • Naweza kupunguziwa bei?
    Ukipenda nguo hiyo na kutaka kuinunua, lakini unataka kupunguziwa bei, unaweza kuuliza: neng da zhe ma? Neng: weza. Da zhe: kupunguza bei. Ma: neno la kisaidizi kwa kuuliza.