Rangi nyekundu ni rangi wanayopenda wachina wengi, katika utamaduni wa China, rangi nyekundu inaonesha baraka na furaha, kwa mfano kila ifikapo sikukuu ya mwaka mpya wa jadi, taa nyekundu hutundikwa kwenye milango ya nyumba kila mahali, na wakati wa sherehe ya kufunga ndoa, bibi harusi huvaa nguo ya rangi nyekundu na viatu vya rangi nyekundu.
Kama mtu fulani amepata mafanikio katika kazi yake tunaweza kusema, yeye "走红了 zou hong le", akiaminiwa na kupendwa na mkuu wake katika kampuni, wengine wanaweza kusema yeye ni "红人 hong ren",akipata faida kutokana na uendeshaji wa ushirikiano wa kampuni, tunaweza kusema yeye amepata "分红 fen hong" , na wanawake wenye sura nzuri wanaweza kuitwa kuwa ni "红颜 hong yan".