Wakati wachina walipokutana na kusalimiana wanaweza kusema : 你好 (ni hao) Habari, Hujambo! Na wakati wa kuagana wanasema: 再见!(zai jian) Kwa heri, tutaonana. Lakini watu wengi wanaposalimiana wanaweza kuulizana: 您去哪儿?(nin qu na er) Unakwenda wapi? 您上班吗 (nin shang ban ma) Unakwenda kazini? 吃饭了吗(chi fan le ma)Umekula? Kuulizana namna hii, watu wa nchi za magharibi huwa hawaelewi ni kwa nini, kwani watu wa nchi za magharibi wanaona mambo kama hayo ni mambo ya mtu binafsi hayafai kuulizwa ovyo. Hivyo watu wa nchi za magharibi wanaposalimiana husema maneno rahisi: Hi, Hello! Good morning! How are you!