Nchini China si wakati wa siku za mapumziko au sikukuu, wala siku za kawaida, jamaa na marafiki wengi wanaweza kwenda kwenye mikahawa kula chakula pamoja, watu wa familia moja moja au marafiki kadhaa wanaweza kukaa kwenye meza ya duara, na vyakula na vitoweo huwekwa katikati ya meza, kila mtu anaweza kuchukua anachopenda. Kama kuna mgeni, mwenyeji hutumia vijiti vya kulia kumchukulia mgeni chakula. Zamani mwenyeji hutumia vijiti vya kulia alivyotumia yeye mwenyewe kumchukulia mgeni chakula, lakini siku hizi wachina wamezoea kutumia vijiti vya kulia vinavyotumiwa kwa ajili ya kuwachukulia wageni vyakula.
Kwenye mikahawa nchini China, wahudumu huleta kwanza vyakula na vitoweo mbalimbali, mwishoni ni supu na matunda.