somo 3 furaha ya siku ya kuzaliwa

 ongea na CRI
 

  • Nakutakia heri ya siku ya kuzaliwa!
    kama ukienda kushiriki kwenye sherehe ya siku ya kuzaliwa ya rafiki yako, utampongeza na kusema "Tunakutakia heri ya siku ya kuzaliwa kwako". Kwa Kichina unasema"zhù nǐ shēng rì kuài lè!"
    "zhù": -takia; "nǐ": wewe; "shēng rì": siku ya kuzaliwa;"kuài lè": furaha.
    Na jibu la sentensi hiyo linaweza kuwa "xiè xiè", ambayo tumejifunza kwenye kipindi kilichopita.

  • Tunywe!
    Tunaposherehekea siku ya kuzaliwa huwa tunaweza kuwaalika marafiki zetu. Na wakati huo tunaweza kunywa vinywaji au pombe. Wakati huo wachina hupenda kuinua glasi na kusema "gān bēi", tunywe.

  • Namba ya simu yako ni nini?
    Baada ya kumalizika kwa sherehe, marafiki walipoagana na kuondoka, huenda unataka kukumbuka namba ya simu ya rafiki mpya, unaweza kuwauliza: "nǐ de diàn huà hào mǎ shì duō shǎo?" Namba ya simu yako ni nini?
    "nǐ de": yako; "diàn huà":simu; "hào mǎ": nambari; shì duō shǎo: "ni ngapi". "nǐ de diàn huà hào mǎ shì duō shǎo?" Nambari ya simu yako ni nini?

  • moja-mbili-tatu-nne-tano-sita-saba-nane-tisa-kumi
    "líng": sifuri , "yī": moja; "èr": mbili, "sān": tatu; "sì": nne; "wǔ": tano; "liù": sita; "qī": saba; "bā": nane; "jiǔ": tisa; "shí": kumi.