Katika China, kuuliza umri wa watu ni jambo la kawaida. Na pia inaonesha unamjali. Kwa mfano, watu humwuliza mzee umri wake kwa kusema:"níng gāo shòu?" Maana yake ni "Una umri gani?" Hii inaonesha unamheshimu mzee. Hivi sasa, vijana wengi wana kazi nyingi, na hawana wakati wa kutafuta mchumba. Huenda wanafanya vizuri kazini, lakini wazazi wao wanawashinikiza kutafuta wachumba mapema. Hivyo, labda hawapendi kuulizwa umri.