Nchini China kama unataka kwenda sehemu nyingine kutalii, mbali na kujiunga na ujumbe wa shirika la utalii, pia unaweza kutafuta shirika la utalii kukusaidia kuagiza hoteli, ama unaweza kuagiza hoteli kwa kupigia simu na kwa kutumia mtandao wa internet. Katika miji mikubwa mbalimbali, mbali na mahoteli, pia kuna mahoteli safi na ya bei nafuu. Pia kuna majumba ya makazi yenye mikahawa, ukikaa ndani ni rahisi kupata malazi na chakula. Kama utakwenda kwenye vijiji vilivyoko nje ya miji, unaweza kupanga chumba kwenye mahoteli madogo yanayoendeshwa na wakulima wenyewe.