Nchini China kuweka akiba benkini ni desturi moja ya wachina, na katika miaka mingi iliyopita, serikali pia iliwataka watu waweke akiba benkini. Tokea China ianze kutekeleza sera ya mageuzi na ufunguaji mlango, watu wengi wamebadilisha mtizamo wao, baadhi yao wameanza kununua hisa, bima au kununua nyumba, ambao wanataka kupata faida nyingi zaidi. Lakini hivi sasa kuweka akiba benkini bado ni njia kuu ya kushughulikia ziada ya mapato kwa watu wengi nchini China.